Pages

Monday, February 11, 2013

mafuta ya kupika aina ya mawese yamsababishia kifungo cha miaka 10 gerezani mtu na mke wake



Mkazi wa mtaa wa migombani wilayani Kibondo mkoani kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja duka na kuiba mafuta ya kupika aina ya  mawese yenye thamani ya shilingi laki moja na elfu ishirini

Mbele ya hakimu wa wilaya ya Kibondo bw Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw Fadhil Noel Tambale amemtaja mtu huyo kuwa ni bw Hayanitishi Bunyenyeri mwenye umri wa miaka 29 na kwamba alishirikiana na mke wake bi Fatma Petro mwenye umri wa miaka 30

Bw Tambale amesema kuwa mnamo Juni 9 , 2012 majira ya saa 1 asubuhi katika eneo la soko la wakulima kabwigwa wilayani Kibondo kwa pamoja watuhumiwa wote wawili ambao ni mke na mme walivunja duka na kuiba mafuta aina ya mawese mali ya bw Yasin Salum

Baada ya upelelezi wa shauri hilo kukamilika hakimu wa wilaya ya Kibondo bw Erick Marley ametoa hukumu kwa mtuhumiwa namba moja ambaye ni bw Hayanitishi Bunyenyeri  ya miaka mitano kwa kosa la kuvunja na kosa la  kuiba miaka 5 jumla atapaswa kutumiakia miaka 10 gerezani

Aidha mtuhumiwa namba mbili  bi Fatma Petro ambae ni mke wa mtuhumiwa namba moja ameepuka kifungo hicho na kuamriwa kutumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kujitetea kuwa ana watoto wadogo ambao anapaswa kuwalea MWISHO

No comments:

Post a Comment