Pages

Tuesday, November 25, 2014

Mbunge Jimbo la Muhambwe Kizimbani kwa kuzuia uandikishaji wapiga kura



 
mbunge jimbo la muhambwe bw felix mkosamli akisisitiza jambo mara baada ya kutoka mahakamani kwa dhamana
Na Mwemezi Muhingo Kibondo

Mbunge wa jimbo la Muhambwe mkoani kigoma Bw. Felix Mkosamali amefikishwa katika mahakama ya wilaya ua kibondo mkoani kigoma akikabiliwa na shitaka la kumzuia karani muandikisha wapiga kura kuto endelea kufanya kazi ya kuandikisha wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa  katika kitongoji cha  Nduta Kijiji cha kumhasha Kata ya Murungu  wilayani kibondo.


Mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo, Bw. Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw.Peter Makala amesema tukio hilo limetokea nov.24 alipofika katika kituo hicho nakuzuia wasiendelee kuwaandikisha wananchi na kwamba hali hiyo ni ukiukaji wa sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa.


 Bw.makala amesema kitendo cha kuwazuia wananchi hao kujiandikisha kwamba ni kuwanyima haki yao ya msingi ambapo wananchi baada ya kuwazuia waliendelea kudai kujiandikisha  lakini hata hivyo mbunge huyo alizuia kabisa kutoendelea na kazi hiyo.


Mshitakiwa amekana shitaka hilo ambapo Hakimu wa mahakama ya wilaya Bw.Erick Marley baada ya kusikiliza pande zote mbili ameiahirisha kesi hiyo mpaka Desemb.29,2014 ambapo kesi hiyo itatajwa tena na mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti kwa kudhaminiwa na watu wawili kila mmoja sh million 2 jumla yake sh million 4.


Katika eneo la mahakama hiyo ilifurika watu mbalimbali kutoka sehemu tofauti waliofika kusikiliza kesi hiyo ambapo hali ya ulinzi  ilikuwa imeimalishwa kwa kiasi kikubwa ilikusitokee vurugu zozote pale na utulivu ulikuwepo..


Awali ilidawa kuwa Mbunge huyo alimnyang’nya kalani huyo Vitabu na Madodoso yote na kuamua kuondoka nayo na kuyapeleka katika ofisi ya mkurugenzi mtenda wa Halmashauri ya wilaya hiyo kinyume taratibu  na baadae kukamatwa na Polisi hadi leo aliopfikishwa mahakamani

Mwisho

No comments:

Post a Comment