Pages

Friday, February 26, 2016

miaka mitano gerezani kwa kukutwa na lita 500 za pombe haramu aina ya gongo




Mkazi wa kata ya mabamba wilayani kibondo mkoani kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kukili kosa la  kukutwa na pombe haramu aina ya gongo kiasi cha lita 500 yenye thamani ya shilingi laki saba na nusu

Mbele ya hakimu mkazi, mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Erick Marley mwendesha Mashitaka wa polisi bw Peter Makala amemtaja mtu huyo kuwa ni Pius John mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa kata ya mabamba

Aidha bw Makala amesema kuwa usiku wa kuamkia leo February 25 mwaka huu kulipatikana taarifa za siri kuwa bw John ana stoo kubwa ya pombe hiyo na baada ya polisi kupata taarifa hizo mkuu wa polisi tarafa ya mabamba bw Fortunatus Rugumamu akishirikiana na serikali ya kijiji walifanya upekuzi na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na pombe hiyo haramu ikiwa kwenye vyombo mbali mbali kama madumu , ndoo na diaba

Baada ya kukamatwa bw pius John amehojiwa na kukili kuwa pombe hiyo ni mali yake na alikuwa akiuza yeye mwenyewe  mbele ya uongozi wa serikali ya kijiji na polisi lakini pia mahakamani

Aidha baada ya mtuhumiwa kukili kosa Mwendesha mashitaka wa polisi bw piter Makala ameiomba mahakama impe adhabu kali mtuhumiwa kwa kuwa pombe hiyo huangamiza maisha ya watu wengi hapa nchini na kupunguza nguvu kazi ya taifa hivyo adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wengine wanaoshughulika na kazi hiyo 

Mahakama ya wilaya ya kibondo ikiongozwa na hakimu mkazi mfawidhi bw Erick Marleye imemhukumu bw Pius John Kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kukili kutenda kosa hilo  ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na biashara haramu ya kuuza pombe zilizopigwa marufuku na serikali

Baada ya kutoa hukumu hiyo hakimu maley ameagiza pombe hiyo haramu iteketezwe na jeshi la polisi chini ya usimamizi wa mkuu wa upelelezi wa jeshi la polisi wilaya ya kibondo bw Twaha Rule na taarifa ya uteketezwaji wa pombe hiyo haramu irudishwe mahakamani





No comments:

Post a Comment