Pages

Wednesday, December 5, 2012

tume iliyoundwa kuchunguza sakata linalowahusu askari polisi wanne juu ya kesi ya kumpiga na kumnyanganya mama mmoja pesa kiasi cha shilingi milioni mbili kutolewa majibu ya tume mwishoni mwa mwezi huu

bi jenisia minani



Tume iliyoundwa kuchunguza askari polisi wanne waliotuhumiwa kumpiga na kumpora mama mmoja pesa kiasi cha shilingi milioni mbili katika tarafa ya Kifura wilayani Kibondo imekabidhi taarifa kwa mkuu wa mkoa wa kigoma na itasomwa mwishoni mwa mwezi huu mbele ya wananchi wa kifura

Ameyasema hayo mkuu wa wilaya ya Kibondo wakati akitoa taarifa mbali mbali za majukumu yake katika mkutano wa ziara ya mwenyekiti wa ccm mkoa uliofanyika katika uwanja wa vijana wilayani hapa

Aidha bw Mwamoto amesema kuwa taarifa ya tume hiyo ilishindwa kutolewa mapema kwa wananchi kutokana na mkuu huyo wa mkoa bw Salehe Issa Machibiya kuwa likizo
Na kwamba alipenda kuisoma yeye mwenyewe mbele ya wananchi kwa kuwa suara hilo limeonekana kuwa la kisiasa zaidi


Bi Jenisia Minani mkazi wa tarafa ya kifura alivamiwa kupigwa na kunyang’anywa pesa kiasi cha shilingi milioni mbili mwishoni mwa mwezi September na watu waliodhaniwa kuwa ni maasikari hali iliyopelekea mkuu wa wilaya ya Kibondo kuunda tume ya kuchunguza sakata hilo MWISHO

No comments:

Post a Comment