Pages

Tuesday, August 11, 2015

Victor Valdes ataja mtu pekee anayeweza kuishi nae

Ikiwa zimepita wiki kadhaa toka golikipa wa Manchester United Victor Valdes hashindwe kuwa katika mahusiano mazuri na kocha wake Louis van Gaal ambae ana amini Valdes ni mtovu wa nidhamu, na mchezaji wa aina hiyo hana nafasi katika kikosi chake.
Valdes ameibuka na kukiri kuwa kocha anayeweza kumuongoza ni Pep Guardiola aliyekuwa akimfundisha kipindi yupo katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania, Valdes alishindwa kuelewana na kocha Louis van Gaal baada ya kugoma kucheza mechi na kikosi cha wachezaji wa akiba.

“mimi huwa ni vigumu kuishi na kufanya kazi na mtu asiyenifahamu, hata mke wangu anastahili kupewa taji kubwa, nilikuwa na bahati sana kuishi kwa misimu kadhaa na Guardiola, alikuwa mwalimu wetu siku zote alikuwa na uwezo wa kuwasiliana na kila mmoja wetu na kumuelewa namna alivyo huku akiweza kuzungumza na watu tofauti tofauti katika chumba cha kubadilishia nguo”>>>Valdes



Kufuatia tabia hiyo aliyoionyesha Louis van Gaal hakumjumuisha katika kikosi kilichosafiri kwenda Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Uingereza hivyo huenda ikawa ni ishara ya kuwashiwa taa nyekundu za kuondoka Man United.

No comments:

Post a Comment