Mkazi wa mtaa wa migombani wilayani Kibondo mkoani kigoma
amehukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja
duka na kuiba mafuta ya kupika aina ya mawese yenye thamani ya shilingi laki moja na
elfu ishirini
Mbele ya hakimu wa wilaya ya Kibondo bw Erick Marley
mwendesha mashitaka wa polisi bw Fadhil Noel Tambale amemtaja mtu huyo kuwa ni
bw Hayanitishi Bunyenyeri mwenye umri wa miaka 29 na kwamba alishirikiana na
mke wake bi Fatma Petro mwenye umri wa miaka 30
Bw Tambale amesema kuwa mnamo Juni 9 , 2012 majira ya saa 1
asubuhi katika eneo la soko la wakulima kabwigwa wilayani Kibondo kwa pamoja
watuhumiwa wote wawili ambao ni mke na mme walivunja duka na kuiba mafuta aina
ya mawese mali
ya bw Yasin Salum
Baada ya upelelezi wa shauri hilo kukamilika hakimu wa
wilaya ya Kibondo bw Erick Marley ametoa hukumu kwa mtuhumiwa namba moja ambaye
ni bw Hayanitishi Bunyenyeri ya miaka
mitano kwa kosa la kuvunja na kosa la kuiba miaka 5 jumla atapaswa kutumiakia miaka
10 gerezani
Aidha mtuhumiwa namba mbili bi Fatma Petro ambae ni mke wa mtuhumiwa namba
moja ameepuka kifungo hicho na kuamriwa kutumikia kifungo cha nje cha mwaka
mmoja baada ya kujitetea kuwa ana watoto wadogo ambao anapaswa kuwalea MWISHO
No comments:
Post a Comment