Pages

Showing posts with label kibondo moto. Show all posts
Showing posts with label kibondo moto. Show all posts

Saturday, November 30, 2013

mkuu wa wilaya ya kibondo agawa mbolea kwa wazee

bw Venance Mwamoto akisoma majina ya wazee wenye sifa za kupata mbolea hiyo



KIBONDO

Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto amegawa mifuko 78 ya mbolea aina ya Minjingu kwa wazee wapatao 164 wa kijiji cha Kibuye Kata ya Kumsenga  aliyoikamata mwaka jana ikiwa kwenye harakati za kuvushwa nje ya nchi kwa njia za magendo

Bw Mwamoto amesema kuwa ameamua kutoa mbolea hiyo kwa wazee wa kijiji cha Kibuye kwa kuwa ilikamatiwa kijijini hapo mwaka jana kabla ya kuvushwa kwenda nchi jirani ya Burundi ikiwa ni kwa njia za magendo ‘’ nimeamua kugawa mbolea hii kwa wazee kuwa kuwa wao kwanza hawana nguvu na itawasaidia kuboresha mashamba yao na kuongeza kipatocha familia’’ alisema mwamoto 

Bw Mwamoto amesema kuwa ameamua kugawa mifuko 74 kwa wazee kisha kubakiza mifuko mingine minne ya mbolea hiyo kwa ajili ya ushahidi kwa watu wa TAKUKURU pamoja na polisi kama itahitajika kufanya hivyo kwa upelelezi Zaidi wa wahusika wa wizi wa mbolea hiyo

Bw Mwamoto amesema  kuwa alikamata mbolea hiyo mwaka jana mwezi wa katika kijiji cha Kibuye kata kumsenga ikiwa kwenye harakati ya kuvushwa kwenda nchi jirani ya Burundi kwa ajiri ya kuuzwa huko pamoja na kwamba mbolea hiyo ilitolewa kama ruzuku kwa wananchi wa wilaya ya kibondo  

Mmoja wa wazee hao bw Charles Ntambala amesema kuwa amefurahishwa na zoezi hilo na kwamba litakomesha wizi wa mbolea ambao umekuwepo kwa muda mrefu na kusababisha wanyonge kutopata haki yao ya msingi kutokana na kuuzwa kwa matajiri wa nchi jirani ‘’ kama unavyojua ndugu mwandishi hapa ni mpakani mbolea imekuwa ikifanyiwa magendo kwa muda mlefu sana na kusababisha sisi tukose haki yetu ya msingi kutokana na mbolea kuongezeka bei maradufu kutona na kuuzwa nje ya nchi namshukuru sana mkuu wa wilaya haijawahi kutokea tangu niishi kijii hiki’’ alisema mzee huyo  

Bw mwamoto amesema kuwa zoezi la ukamataji mbolea inayofanyiwa magendo litakuw aendelevu ili kukomesha wizi huo unaosababisha wananchi wakose haki yao ya msingi na kudumaza maendeleo kwa watanzania ENDS 






Thursday, November 21, 2013

mme aua mke mtoto akaa na maiti yaya mama yake kwa siku tatu



 
mkuu wa jeshi la polisi wilayani kibondo bw Marko Joshua akifungua mlango katika nyumba aliyokutwa marehemu
 
mwili wa marehemu kama ulivyokutwa chumbani
mtoto aliyeishi ndani na maiti ya mama yake kwa muda wa siku tatu akiwa amebebwa na babi yake

 
pamoja na kukutwa akiwa hai pembeni ya marehem mama yake lakini inaonekana nae alipata suruba kiasi fulani

 
baba mzazi wa kijana aliyetekeleza mauaji

Mwanamke Mmoja Mkazi wa Kijiji cha Mpevyi Kata  ya Busagara Wilayani Kibondo ameuawa kikatili kwa kunyongwa  shingo hadi kufa na  mumewake na mwili wake kukutwa umeharibika vibaya baada ya kuterekezwa kwa kufugiwa ndani kwa siku 3, na mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 5.

Taarifa za awali kutoka kamati ya Ulinzi na usalama ya Kijiji hicho imemtaja aliyeuawa kuwa ni Bi.Anerth Shabani mwenye umri wa miaka 22, akiwa na mtoto wake Lahabu Bugaru mwenye umri wa miaka 5 ambaye amekutwa akiwa hai huku akiwa  amejeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni na mapajani.


Akizungumza na kibondo moto Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bw.  Felix Kabuti amesema tukio hilo limetukia usiku wa November 16 mwaka huu, Nyumbani kwake ambapo imeelezwa kuwa marehemu Anerth shabani ameuawa na mumewake shedrak yoram Chales kwa kumunyongwa kisha kuulaza mwili wake kitandani na yeye kutokomea kusikojulikana baada ya kutekeleza unyama huo

.
Naye diwani wa kata ya Busagara Bw. Godwin Sibanilo amesema awali alipata taarifa kutoka kwa wananchi iliyoashilia kuwepo kwa harufu kali kutoka katika nyumba hiyo ambapo kwa kushirikiana na viongozi walifanikiwa kubomoa mlango na kuingia ndani ambapo walikuta mwili wa mwananke huyo na mtoto Lahabu bugaru aliyekuwa ameulalia mwili wa mama yake.


Ndugu wa mwanamke huyo aliyenyongwa waliruhusu daktari kufanya uchunguzi wa kifo hicho kimesababishwa na nini ambapo pia waliruhusu askari kufanya uchunguzi wao lakini wamegomea mwili huo kuzikwa kwa madai kuwa mwanaume huyo hakuwa ametoa mahali wakati alipomuoa binti yao

Tuesday, November 19, 2013

walemavu wakiwezeshwa wanaweza tuwape nafasi

mkuu wa wilaya ya kibondo bw venance mwamoto akicheza na mlemavu asiyeona ikiwa ni moja wapo ya njia ya kuwapa furaha walemavu



Wito umetolewa kwa serikali kuchukua hatua madhubuti ya kutatua kero mbali mbali zinazowakabili watu wenye ulemavu ikiwemo kuhamasisha wazazi kutowafungia watoto wenye ulemavu ndani  na kushindwa kuwapeleka shule kwa kisingizio cha kuchekwa ama kutengwa na jamii

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa chama cha walemavu wilayani kibondo bw Evalisto Ngalama wakati akizungumza na kibondo moto  na kuongeza kuwa ikiwa walamavu watawezeshwa hasa kupewa mafunzo ya ufundi basi serikali itapunguza watu tegemezi kwa kiasi kikubwa sana

Aidha bw Ngarama amesema kuwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inapaswa kuchukua hatua madhubuti ya kuwasaidia walemavu ili kujenga jamii yenye usawa , upendo , mshikamano pamoja na amani

Bw Ngarama ameema kuwa jamii kwa kushirikiana na serikali, taasisi binafsi inatakiwa kujenga miundombinu rafiki kwa walemavu itakayowarahisishia kupata huduma muhimu za afya na elimu ili kuondokana na adha wanayoipata pindi wanapohitaji huduma hizo. ENDS

Friday, November 15, 2013

Baraza la madiwani wilayani kibondo mkoani kigoma limeketi ikiwa ni kikao cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2013/ 2014








Halmashauri ya wilaya ya kibondo mkoani kigoma imeidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 3 na milioni 347 katika mwaka wa fedha 2013/ 2014 kutoka serikali kuu na wahisani mbali mbali wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoko chini ya kamati ya elimu afya na maji

Mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji bw Ali Amini Gwanko Mpondamali ameyasema hayo wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo katika baraza la madiwani lililoketi leo katika ukumbi wa vijana na kuongeza kuwa fedha hizo ni sawa na asilimia 57.5 ya bajeti yote iliyoidhinishwa

Aidha bw Gwanko amesema kuwa halmashauri ilikuwa imebaki na salio ishia kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kiasi cha shilingi bilioni 3 na milioni 525 hivyo pesa itakayotekeleza miradi mbali mbali katika kamati hiyo kwa mwaka wa fedha 2013/2014 itakuwa zaidi ya shilingi bilioni 6

Amesema kuwa katika utekelezajaji wa miradi mbali mbali kamati ya elimu, afya na maji kwa mwaka wa fedha uliopita ilikabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kuchelewa kuanza kwa mfumo wa EPICA na hivyo kushindwa kufanya malipo kwa wakandarasi wenye mitaji midogo hivyo kukwamisha kazi

Monday, November 11, 2013

Tamko kutoka kwa Zitto Kabwe kuhusiana na kinachoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema”






NILIPOKUWA katika ziara ya bara la Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba 2 mwaka huu (2013), nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema” ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
“Taarifa ya Chadema inasema kwamba chama hicho (chama changu) kilikuwa kimechunguza mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema.
Ripoti hiyo ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes ambaye, kwa mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 za Marekani kupitia kwenye akaunti yake binafsi.
Taarifa hii ya kutunga na iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha, imenifadhaisha, kunisikitisha na kunikasirisha.
Taarifa hii iliibuliwa katika kipindi ambacho nilikuwa safarini kutetea haki za Watanzania na Waafrika ambao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi mali katika nje za nje na pia kupigania makampuni ya mataifa tajiri yalipe kodi stahiki katika nchi zetu.
Pengine lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni kutaka kunipoteza kutoka katika nia na dhamira yangu ya dhati ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao. Muda ambao watunzi wa ripoti hiyo waliamua kutoa taarifa yao unazua maswali mengi kuliko majibu.
Nafahamu kwamba mimi ni mwanasiasa ambaye nimekuwa mlengwa (target) wa mashambulizi kutoka kwa makundi mbalimbali ya wanasiasa na vikundi vyao. Kama mwanasiasa, niko tayari kupokea changamoto zozote zinazokuja na uanasiasa wangu.
Hata hivyo, ambacho sitakubali ni kwa watu kutumia jina langu na uanasiasa wangu kunichafua mimi binafsi na watu wengine wasiohusika kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo yao ya kidhalimu.
Raia huyo wa Kijerumani tayari amekana kuhifadhi fedha zangu. Kwa maelezo yake kwa baadhi ya viongozi wa Chadema amekana kuwa na akaunti inayotajwa na amekana pia kuwepo nchini Ujerumani katika siku na wakati uliotajwa kwenye ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imemtaja pia mtu kama Dk. Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ikidai kwamba nilikutana naye na alishiriki kwenye igizo hilo la kunipa fedha.
Niseme mapema kwamba tangu kuzaliwa kwangu sijawahi hata mara moja kukutana na Dk. Kimei popote pale ndani au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye amejenga jina lake kwenye taaluma ya kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la kumchafua Zitto Zuberi Kabwe si uungwana bali ni unyama.
Kutokana na uchafuzi huu wa wazi dhidi ya taswira yangu binafsi na watu wengine walioingizwa kwenye mkumbo huu, nimeandika rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa kumwomba athibitishe kwamba kinachoitwa Taarifa ya Siri ya Chadema ni kweli ni taarifa ya chama au kiikanushe ili niweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa hekaya hiyo.
Cha ajabu, nimepokea ujumbe wa kutishiwa maisha kutoka kwa mtu anayejiita Theo Mutahaba na kuahidiwa KUPOTEZWA endapo nitaendelea na jitihada zangu za kupambana na ufisadi na kutafuta haki kwa Watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi, kikanda, kikabila na kidini.
Natarajia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote ambao wamehusika na utungaji na uenezi wa taarifa hii. Nitahakikisha kwamba wahusika wanatafutwa na kufunguliwa mashitaka stahiki ya upotoshaji na kuchafuana.
Ni matarajio yangu kwamba wale wenye mapenzi mema na Tanzania, mimi binafsi na utawala wa sheria, wataelewa nia yangu ya kutafuta haki katika suala hili.
Nimeamua kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Watanzania na kama alivyopata kusema Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela; “Struggle Is My Life.”
Forward Ever, Backward Never- Kwame Nkrumah

Friday, September 27, 2013

vijana oparation miaka 50 ya jkt wamehitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika kambi ya jkt kanembwa






mkuu wa kikosi namba 824 jkt kanembwa meja Elasmos Bwegoge

luten kanal MB Hiki mwakilishi wa mkuu wa jeshi la kujenga taifa