Mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya kati imeteketeza
tani moja na nusu ya bidhaa zisizofaa
kwa matumizi ya binadamu bidhaa ambazo zimekusanywa kutoka maduka mbali mbali
yaliyoko katika wilaya za kakonko na kibondo
Mkaguzi wa chakula kutoka mamlaka ya chakula na dawa TFDA
kanda ya kati bw Abel Dauda amesema kuwa
ofisi ya mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya kati katika kutekeleza mpango
kazi wake kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2013/14 imefanya ukaguzi katika
halmashauri za wilaya ya kibondo na kakonko kwa kushirikiana na ofisi za
waganga wakuu wa halmashauri husika
Kwa upande wake afisa afya mazingira wilayani kibondo bw
joseph kalobagwa amesema kuwa elimu huotolewa kila wanapotembelea maduka mbali
mbali ili kuhimiza kuacha tabia ya kuagiza bidhaa zisizo faa kwa matumizi ya
binadamu
Mmoja wa wafanyabiashara wilayani kibondo bw musa hamisi
ameitaka mamlaka ya chakula na dawa kudhibiti wafanyabiashara wakubwa kwa kuwa
wao ndio husambaza bidhaa zisizo na ubora kwa wafanya biashara wadogo
Ukaguzi huo uliofanywa na TFDA kanda ya kati ulilenga
kuangalia utekelezaji wa sheria ya chakula dawa na vipodozi namba moja ya mwaka
2003 katika udhibiti wa ubora usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula dawa vipodozi na vifaa tiba
No comments:
Post a Comment