Pages

Monday, March 4, 2013

miezi 12 jela kwa kosa la kuiba mihogo

KIBONDO

Mkazi wa kijijii cha kitahana wilayani kibondo mkoani kigoma  amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela baada ya kukili kosa la kuiba mihogo yenye thamani ya shilingi laki nane

Mbele ya hakimu wa wilaya ya kibondo bw Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw Fadhili Noeli Tambale amemtaja mtu huyo kuwa ni bw Sunzu Kasase mwenye umri wa miaka 68

Bw Tambale amesema kuwa mnamo February 24 , 2013 majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha kitahana bw Kasase aliiba mihogo iliyokuwa tayari imevunwa na wanakikundi cha KIBASO hivyo kusababisha hasara ya shilingi laki nane mali ya KIBASO GROUP

Hakimu wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Erick Marley ametoa hukumu ya kutumikia miezi 12 jela kwa bw Sunzu Kasase mwenye umri wa miaka 68 kuanzia leo marchi 4 , 2013 baada ya ushahidi wa kosa hilo kujitosheleza  MWISHO

No comments:

Post a Comment