Tuesday, December 16, 2014
kauli ya serikali kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa
Kufuatia dosari nyingi zilizojitokeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika maeneo mengi nchini Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia amesema wote waliohusika kuvuruga uchaguzi huo kwa watawajibishwa hata kama ikiwa ni yeye au ofisi yake.
“Tumesema tutafanya uchunguzi na ikibainika kwamba kuna mtu amekosea kwa nafasi yake kule kwenye Halmashauri tutawachukulia hatua, je ikibainika ni mimi ambae nimevuruga niko tayari kuwajibika, kama itabainika kuna Halmashauri haikufanya vizuri kwa sababu mimi ndio nimewafanya wasifanye vizuri nitawajibika, lakini kama ni wao wenyewe tumewapa maelekezo yote ya kufanya na wao wamevuruga wao tutawawajibisha…” — Waziri Hawa Ghasia.
Wakati huo huo amesema kuwa katika miaka ijayo uchaguzi huo utakuwa chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, huku akiongeza kuwa uchaguzi huo umekuwa na changamoto mbalimbali.
Hapa kuna sauti nilikurekodia wakati Televisheni ya ITV ikiripoti kuhusu taarifa hiyo.
usikose kutembelea blog yako kibondo moto kwa habari moto moto kila siku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment