Walimu wametakiwa kuiona kazi ya ualimu kuwa ni wito ili kufanya kazi hiyo kwa bidii na moyo wa kujituma pamoja na nia ya kuwasaidia wanafunzi hali itakayosaidia kuinua kiwango cha elimu na ufauru mzuri
Ameyasema hayo mgeni lasmi padre Christopher Ndizeye paroko wa parokia ya Kibondo katika mahafari ya 9 ya kidato cha sita shule ya sekondari ya wasichana Bon Konsili yaliyofanyika katika ukumbi wa shule hiyo iliyoko kata ya mabamba wilayani Kibondo
Aidha padre Ndizeye amesema kuwa mwalimu anapaswa kujitoa kwa ajili ya shule na wale anaowafundisha hali itakayosaidia wanafunzi kupenda masomo yao na hatimae kuinua kiwango cha taaruma
Mkuu wa shule hiyo ya wasichana bon konsil sisita Generoza Mpilirwe amewataka Wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwalaumu walimu pale watoto wao wanapokuwa wamefeli mtihani bali wajenge tabia ya kuwafunza nidhamu kwa kuwa nidhamu ndio msingi wa maendeleo mazuri ya mwanafunzi
Katika risala iliyoandaliwa na wahitimu na kusomwa na Tekla mchunguzi kwa kiingereza kisha ikasomwa na Juliana Bagamba kwa Kiswahili wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazopelekea kushindwa kujisomea kwa wakati likiwemo suala zima la ukosefu wa nishati ya umeme
Mkuu wa wilaya ya Kibondo ambaye alikuwa mgeni mwalikwa katika mahafari hiyo ya kidato cha sita ameahidi kutatua tatizo la umeme ambapo baada ya kukamilika katika mji wa kibondo hatua itakayofuata ni kupeleka nishati hiyo katika kata ya Mabamba na Busunzu
Mzee faransisi mkosamali yeye aliwakilisha wazazi katika sherehe hizo za kuwaaga wahitimu wa kidato cha sita bon konsil
Wanafunzi 37 kati ya 41 walioanza kidato cha tano wamehitimu elimu ya kidato cha sita katika shule ya wasichana Bon Konsil wakiwa wamefanikiwa kufanya vizuri katika mitihani yao ya moko wakshika nafasi ya pili kimkoa MWISHO
No comments:
Post a Comment