Wakazi wa kijiji cha kigendeka ambao ni zaidi ya 9800
wanategemea visima viwili vya maji hali inayowalazimu kutumia zaidi ya masaa 6
kila siku kututafuta huduma ya maji hali ambayo imepelekea shughuli za
maendeleo kukwama kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta huduma hiyo
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakizungumza na gazeti la
kigoma yetu wamesema kuwa tatizo la maji
kijijini hapo limedumu kwa muda mrefu kutokana na baadhi ya visima kuharibika
huku visima vingine vikitoa maji kwa uchache hali ambayo huwalazimu kukaa kisimani
kwa muda mrefu
Perajia John, Jacklina madabanga pamoja na Abdul Chubwa
wamesema kuwa tatizo la maji katika kijiji cha kigendeka ni kubwa hivyo ni vema
serikali ikafanya mchakato mapema ili kunusuru hali ya wananchi kutumia muda
mwingi kutafuta huduma ya maji hali inayoathili maendeleo yao
Gazeti la kigoma yetu lilikuta baadhi ya wanafunzi wakichota
maji katika moja ya kisima ambacho hutumia Zaidi ya dakika kumi kujaza ndoo
moja na mwanafunzi Elizabeth Mibara alipohojiwa amesema kuwa kukosekana kwa
maji kuna waathili sana wanafunzi kwa kuwa hulazimika kukatiza masomo ili
wakatafute huduma ya maji hali ambayo inawaathili pia kitaaruma
Aidha mwenyekiti wa kijiji cha Kigendeka bw Yotham Kitwe
amesema kuwa halimashauri ya kijiji hicho tayari imejadili na kupitisha swala
la wananchi kuchangia shilingi mia tano mia tano kwa ajili ya ukarabati wa
visima vibovu na tayari serikali ya kijiji imechangia shilingi laki nne kutoka
vyanzo vyake vya ndani kwa ajili ya kuanza kukarabati baadhi ya visima vibovu ambapo
mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi march tatizo hilo litakuwa limeanza kutatuliwa
Afisa mtendaji wa kata ya Busagara bw Baruan Gwimo amekili
kuwepo kwa tatizo hilo katika kijiji cha kigendeka na kwamba swala hilo
limewekwa katika mipango ya kamati ya maendeleo ya kata kwa mwaka wa fedha
2015/2016 ambapo pia baadhi ya mashirika
yasiyo ya kiserikali yameombwa kusaidia
kutatua kero ya amaji katika kijiji hicho
No comments:
Post a Comment