Pages

Sunday, April 26, 2015

miaka 45 jela kwa kulawiti mtoto wa miaka 10

mtuhumiwa wa kesi ya ulawiti



KIBONDO

 Mkazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Kibondo mkoani Kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 45 jela baada ya kukutwa na hatia katika  kosa la kumkamata kwa nguvu na kumlawiti  mtoto wa miaka 10 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Bitare


Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya hiyo bw Ismail Ngaile, mwendesha mashitaka wa Polisi Bw, Andulile John  amemtaja mshitakiwa huyo kuwa ni Masumbuko  Adam, miaka 35 mkazi wa mtaa wa Maragalasi na kwamba alitenda kosa hilo mnamo march19.2015 katika kijiji cha Bitare alikokuwa anafanya biashara ya kununua vyuma chakavu


bw Andulile amesema kuwa tarehe hiyohiyo majira ya saa moja jioni, katika kjiji cha Bitare wakati mtoto huyo alipokuwa ametumwa na Baba mzazi kumsalimia Bibi yake ndipo mtuhumiwa alimkamata kwa nguvu mvulana huyo na kumvutia kwenye shamba la migomba na kumtendea kitendo hicho cha kinyama kwa kumlawiti katika njia ya haja kubwa na mdomoni, 


baada ya ushahidi kujitosheleza upande wa mashitaka uliomba adhabu kali itolewe ukilejea kesi ya nguza Viking kwa jina maarufu babu seya na wenzake dhidi ya jamuhuri kesi iliyoamuliwa na mahakama ya rufaa ambapo washitakiwa walihukumiwa kifungo cha maisha jela 


baada ya upelelezi kukamilika bila kuacha shaka lolote mahakama ya hakimu mkazi imezingatia maombi ya upande wa mashitaka na kumuhukumu mshitakiwa huyo bw Masumbuko Adam kifungo cha miaka 45 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kulawiti ama kuingilia watoto kinyume na maumbile ENDS

No comments:

Post a Comment