Pages

Thursday, August 30, 2012

wanawake washauliwa kujitokeza kutoa maoni katiba mpya

wanawake washauliwa kujitokeza kwa wingi kuchangia maoni ya katiba 

  akina mama wilayani kibondo wakiuza mazao yao bila kuwa na bei maalum kila mtu akiuza kwa bei anayoitaka kitu kinachosabisha walanguzi kuwakandamiza wakulima haya ni baadhi ya mambo ambayo wangeyasema ili yaingie kwenyi katiba mpya lakini wamekuwa hawajitokezi kutoa maoni yao (picha na james jovin)


KIBONDO
Wanawake mkoani  Kigoma  wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni wakati tume ya mabadiliko ya katiba itakapokuwa ikipita katika maeneo yao  hata kama hawajui katiba iliyopita kwa kuwa maoni hayo si lazima yatokane na katiba ya sasa bali kuangalia changamoto katika maeneo wanayoishi.  

Bi Mwatum Malale ambaye ni mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba ameyasema hayo alipokuwa akiongea na radio kwizera na kuongeza kuwa ni vema wananchi wakijitokeza kwa wingi katika kuchangia katiba hiyo kwa kuwa ni suala la kihistoria linalojitokeza mara moja baada ya miaka mingi

Bi Malele pamoja na mambo mengine ameshauri akina mama kutoa michango yao na si kutazama tu wengine wakichangia maoni kwenye katiba ya nchi hii kwa kuwa ni suala la kihistoria ambalo huja mara moja baada ya muda mlefu na kwamba maoni yote yatakayotolewa yatafanyiwa kazi bila kujali kama yanapatikana katika katiba ya sasa

Bi malale amewataka wananchi kusema mambo wanayohisi yanaweza kuingia kwenye katiba kwa kuwa yanaweza kusaidia katika kuandika katiba mpya kutokana na kuwa tume hiyo itafahamu kwa undani ni mambo gani wananchi hawapendi na mambo wanayopenda

Tume ya mabadiliko ya katiba kwa hivi sasa iko mkoani kigoma ambapo hii leo imeanza kukusanya maoni katika kata za wilaya ya kakonko ambapo tarehe 31 agost mpaka tarehe 3 septemba watakuwa katika kata za wilaya ya kibondo MWISHO

No comments:

Post a Comment