Pages

Sunday, September 9, 2012

usafirishaji haram wa binadamu kibondo kikwazo kwa viongozi

mkuu wa wilaya ya kibondo bw venance mwamoto akiwa amesimama na vijana waliokuwa wanasafirishwa kutoka burundi


KIBONDO   
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Kitema kata ya Nyakitonto anashikiliwa na idara ya uhamiaji wilayani kibondo mkoani kigoma kwa kosa la usafirishaji haramu wa binadamu ambapo mtu huyo alikamatwa akisafirisha vijana 7 kutoka Burundi akiwa peleka wilayani Kasulu mkoani kigoma kwa ajili ya kuwafanyisha kazi ya kuchunga ngombe

Afisa uhamiji wilayani kibondo bw Njunwa Mlaki amemtaja mtu huyo kuwa ni bw Yolam Venance mwenye umri wa miaka 26 na kwamba mtu huyo alikamatwa na bw  Rogetho Bathoromew ambaye pia ni afisa uhamiaji baada ya kutalifiwa na wananchi wazalendo

Aidha bw Mlaki amesema kuwa bw Venance alikuwa akisafirisha watu 7 ambao wote wana umri chini ya miaka 17 kutoka kijiji cha Kabuyenge wilaya ya  Gisuru nchini Burundi kuwapeleka wilayani Kasulu kwa ajili ya kufanyishwa kazi za kuchunga ngombe ambapo ni kinyume na sheria za uhamiaji

Mtuhumiwa huyo bw Yolam Venance bado anashikilwa na kwamba atakapelekwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa shitaka linalomkabili baada ya upelelezi kukamilika

Baada ya kukamatwa kwa vijana hao mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto akiwa ameambatana na maofisa uhamiaji wamewasafirisha vijana hao mpaka mpakani mwa Burundi na Tanzania ambapo vijana hao wamewakabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Gisuru nchini Burundi bw Ndikuliyo Egide kwa ajili ya kuwarudisha nyumbani kwao  MWISHO
mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance mwamoto (kati kati) akiwa na viongozi kutoka burundi waliofika mpakani ili kukabidhiwa vijana waliokuwa wakisafirishwa kwenda wilayani Kasulu



vijana waliokuwa wakisafirishwa kutoka Burundi wakiwa kwenye gari la maofisa wa uhamiaji tayari kwa kurudishwa nchini kwao .

No comments:

Post a Comment