Pages

Sunday, April 26, 2015

AKUTWA AMEJINYONGA NDANI YA NYUMBA , MWILI WAKUTWA CHINI KAMBA ILIKATIKA

mtoto wa marehemu akielezea mambo yalivyokuwa



Mkazi wa kitongoji cha kumwerulo katika mamlaka ya mji mdogo wa kibondo mkoani kigoma bw Makutenda Ntikahela amekutwa amefariki dunia hapo jana april 25, 2015 baada ya kujinyonga kwa kutumia Kamba ya mbuzi akiwa chumbani kwake na kwamba huenda alijinyonga Zaidi ya siku tatu zilizopita kutokana na kwamba mwili ulikuwa umeanza kuharibika

Akizungumza na kibondo moto  mtoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la marogo makutenda amesema kuwa baba yake alikuwa anaishi peke yake katika nyumba hiyo baada ya kuwafukuza yeye na mama yake Zaidi ya miezi miwili iliyopita hivyo alipokuja kumuangalia alikutana na harufu kaali kuingia ndani akakuta tayari baba amejinyonga Zaidi ya siku tatu kwa kuwa mwili ulikkuwa tayari umeanza kutoa harufu kali

Mke wa marehemu amesema kuwa baada ya kufanyiwa fujo na mme wake Zaidi ya miezi miwili iliyopita aliamua kuondoka na kumuacha mme akiishi peke yake ambapo yeye alienda kuishi katika nyumba ya dada yake na mme wake huku akisubiri mambo yatulie ili aweze kurudi kwa mme wake lakini mambo yakawa tofauti akapewa taarifa kuwa mme wake amejinyonga

Mdogo wake na marehemu aliyejitambulisha kwa jina la mtokile ntigahela amesema kuwa marehemu alikuwa na tabia ya kusema kuwa iko siku atajinyonga hivyo hawawezi kumtuhumu mtu yeyote kutokana na kifo hicho kwa kuwa alikuwa akilewa pombe mambo yanakuwa tofauti hata historia inaonyesha kuwa baba yake na marehemu nae alikufa kwa kujinyonga miaka mingi iliyopita

Mwenyekiti wa kitongoji cha kumwerulo bw magaka mathey amesema kuwa huenda marehemu alijinyonga Zaidi ya siku tatu zilizopita kwani majirani ndio waliogundua baada ya kusikia harufu kali ikitokea ndani ya nyumba na kumtaarifu ambapo walipoangalia ndani walikkuta Kamba aliyotumia kujinyongea imekatika na mwili umedondoka chini

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya kibondo dr kizito ruhamvya alifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi juu ya nini hasa chanzo cha kifo cha marehemu na amebainisha kuwa marehemu alikufa kwa kujinyonga kwani hakuna jeraha lolote alilokutwa nalo Zaidi ya Kamba shingoni ENDS 





No comments:

Post a Comment