Pages

Tuesday, August 21, 2012

mchezaji afia uwanjani wilayani kibondo akiitumikia timu yake


Hapo jana katika ufunguzi wa michuano ya ligi ya jamii wilayani kibondo mkoani kigoma  imetokea habari za kusikitisha ambapo  aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari  kanyamahela amefaliki dunia baada ya kuanguka chini akiwa mchezoni ambapo alikuwa akiitumikia tumu yake ya kazilamihunda iliyokuwa ikicheza dhidi ya chilambo katika kata ya kasanda  
Akiongea na radio kwizera kwa njia ya simu afisa mtendaji wa kata ya kasanda bw Boniface kibada amemtaja mwalimu huyo kuwa ni innocent tumaini Daniel ambaye alikuwa mzaliwa wa  kazilamihunda
Kaktibu wa chama cha mpira wa miguu hapa wilayani kibondo bw james samsoni  ameelezea kuhusu kifo hicho na kuelezea taratibu za mchezo wa mpira wa miguu mchezaji anapokuwa amefia uwanjani
Hizo zilikuwa ni taarifa za majonzi zinahusu mchezo wa mpira wa miguu ambapo mwalimu innocent Samson amefia uwanjani akiitumika timu yake ya kazilamihunda  katika michuano ya ligi ya jamii
Katika kituo cha kibondo michuano hiyo ya ligi ya jamii ilianza tarehe 20 julaya ambapo kanyamahela ilimenyana na mugoboka ambapo matokeo ya mchezo huo ni kwamba timu hizo zilitoka sale ya goli moja kwa moja mfunguaji wa kanyamahela alikuwa devidi titusi dakika ya 14 na mugoboka aliyefunga alikuwa ni  john pius dakika ya  39

Mechi iliyofuatia ilikuwa baina ya migombani futboll clab dhidi ya bitale football klab na matokeo ya mechi hiyo ni kwamba migombani

1 comment: