Pages

Friday, November 22, 2013

aokota Siraha kisha aisalimisha




Mkazi wa kata ya mabamba wilayani kibondo mkoani kigoma ameokota siraha aina ya SMG alipokuwa akilima shambani kwake ikiwa na lisasi 26 pamoja na magazine moja kisha kuisalimisha serikali ya kijiji

Siraha hiyo imeokotwa na mkazi wa kitongoji cha Kijangala kijiji cha Mkalazi kata ya Mabamba bw Moshi Razalo mwenye umri wa miaka 24 jumanne hii ya Novemba 19 ambapo siraha hiyo ilikuwa imefungwa kwenye suruali ya kijeshi kisha kuchimbiwa ardhini

‘’Nilikuwa nalima shambani kwangu sasa nikasikia kama jembe linakwama kwenye kitu kigumu nilipofukua ndio nikaona suruali ya kijeshi kuangalia nikakuta kuna siraha pamoja na lisasi zipatazo 26 basi ikabidi nivisalimishe serikali ya kijiji alisema bw Moshi Razalo

Aidha Bw Razalo amesewataka raia wema kusalimisha siraha ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mara tu waonapo ama kuhisia mtu yeyote mwenye kumliki siraha kinyume cha sheria ili kuimarisha usalama wa raia na mali zake kwa maendeleo ya jamii

Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto pamoja na mkuu wa jeshi la polisi bw Marko Joshua walipigiwa simu mara baada ya siraha hiyo kusalimishwa kwa serikali ya kijiji kisha kuchukua uamuzi wa kuifuata siraha hiyo  na kuihifadhi kituo cha polisi kibondo  
‘’ ilibidi nimpigie simu mkuu wa jeshi la polisi wilayani hapa kisha tukaenda eneo la tukio tukamkuta kijana aliyeokoto bunduki hiyo akaeleza jinsi ilivyokuwa kwa kweli anaonekana ni mzalendo na mimi nitampa motisha ya shilingi elfu 50 ili iwe fundisho kwa wengine unajua SMG ni siraha ya kivita kabisa kwa hiyo kama mtu mwingine angeenda kuitumia tofauti kabisa alisema bw Mwamoto

BW razalo amepatiwa motisha ya shilingi elfu hamsini baada ya kuokota siraha hiyo na kuisalimisha ikiwa ni motisha kwake na kwa watu wengine watakaoona au kutoa taarifa za watu wanaomiliki siraha kinyume cha sheria ENDS  

No comments:

Post a Comment