sensa ya leta kero kibondo
na james jovin
Mkuu wa wilaya ya kibondo bw venance mwamoto hapo jana amelazimika kutoa maelezo mbele ya mamia ya makarani wa sensa waliokuwa wameandamana mpaka kwenye viunga vya halmashauri wakidai pesa zao pamoja na vifaa vya kufanyia kazi ikiwa ni masaa machache kabla ya kuanza kwa zoezi hilo la sense ya watu na makazi
Akiongea mbele ya makarani hao bw mwamoto amewataka kutulia huku wakisubiri mpaka hapo vifaa vitakapokuwa tayari baadae hii hiyo jana majira ya saa kumi za jioni kutokana na vifaa hivyo kuchelewa kufika katika maeneo husika
Akitoa maelezezo hayo juu ya kuchelewa kwa vifaa hivyo kama kawaida yake alianza na slogani yake ya kibondo bila uchafu
Makarani hao wameandamana mpaka kwenye viunga vya halmashauri ya wilaya ya kibondo wakishinikiza kupata vifaa vya kufanyia kazi pamoja na pesa zao kutokana na kuwa makarani wengine wanalazimika kutumia nauli kwa kuwa sehemu walizopangiwa ni mbali
Mpaka blog hii ya habari na michezo inaondoka eneo hilo makarani hao walikuwa wamekubaliana na mkuu wa wilaya kuwa watasubiri vifaa hivyo pamoja na pesa yao kwa ajili ya kwenda kwenye maeneo waliyopangiwa
No comments:
Post a Comment