Pages

Tuesday, September 18, 2012

askari polisi wanne wameshikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kupola sh. milioni mbili

bi Jenisia Minani akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya kibondo baada ya kupigwa na kunyang'anywa pesa shilingi milioni mbili na watu waliodhaniwa kuwa ni mapolisi (picha na james jovin )

KIBONDO
Mtu mmoja mkazi wa kifura kata ya busunzu wilayani kibondo amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo baada ya kuvamiwa , kupigiwa na kunyanganywa pesa kiasi cha shilingi milioni mbili pamoja na simu za mkononi ambapo watuhumiwa ni maaskari polisi wanne waliokuwa dolia katika kijiji cha Mkugwa

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani kibondo na mkuu wa wilaya hiyo bw Venance Mwamoto akiongea na waandishi wa habari amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi usiku septemba 17 katika tarafa ya kifura ambapo aliyevamiwa na kuporwa pesa ni bi Jenisia Minani mwenye umri wa miaka 36

Bw Mwamoto hapo juzi  juma tatu usiku  amelazimika kufunga safari usiku wa manane mpaka eneo la tukio baada ya wananchi hao kusema kuwa hawawezi kutoa ushilikiano wowote bila kumuona mkuu huyo wa wilaya  

Aidha bw MWamoto alifanikiwa kuwatuliza wananchi waliokuwa wamepandwa hasira kutokana na tukio hilo waliokuwa wamefika kituo cha polisi tarafa ya kifura wakiwa na rungu na mapanga kwa kuwachukuwa mapolisi hao na kuwapeleka kituo cha polisi cha wilaya ambapo mama huyo aliyekuwa amepigwa virungu akipelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu

Kwa upande wake mama huyo ambaye mpaka hivi sasa amelazwa katika hospital ya wilaya ya kibondo bi Jenisia Minani  amesema kuwa watu wanne walimvamia wakati akielekea nyumbani akitoka dukani na kwamba walimpiga na kumnyanganya fedha alizokuwa nazo kwenye mfuko wa lambo pamoja na simu ya mkononi
Muuguzi aliyekuwa  zamu  wodi namba tatu katika hospitali ya wilaya ya kibobndo  amesema kuwa mgonjwa huyo anaendelea vizuri na anapata matibabu kama wagonjwa wengine

Aidha mkuu huyo wa wilaya ya kibondo  amekusudia kuunda tume huru ya kuchunguza tukio linalowahusu maaskari polisi wanne la kuvamia na kumnyanganya mama mmoja pesa kiasi cha shilingi milioni mbili
Pamoja na mambo mengine bw Mwamoto amesema kuwa tume hiyo haitahusisha jeshi la polisi kwa kuwa wahusika wa tukio hilo ni polisi wenyewe na kwamba atatafuta watu wengine kutoka idara tofauti kwa ajili ya kuchunguza sakata hilo

  bw venance mwamoto amewataka wananchi walioshuhudia tukio hilo  kumpa ushilikiano ili kubaini chanzo cha tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria  wahusika wa tukio hilo MWISHO

No comments:

Post a Comment