wanawake washauliwa kujitokeza kwa wingi kuchangia maoni ya katiba
akina mama wilayani kibondo wakiuza mazao yao bila kuwa na bei maalum kila mtu akiuza kwa bei anayoitaka kitu kinachosabisha walanguzi kuwakandamiza wakulima haya ni baadhi ya mambo ambayo wangeyasema ili yaingie kwenyi katiba mpya lakini wamekuwa hawajitokezi kutoa maoni yao (picha na james jovin)
KIBONDO
Wanawake mkoani
Kigoma wametakiwa kujitokeza kwa
wingi katika kutoa maoni wakati tume ya mabadiliko ya katiba itakapokuwa
ikipita katika maeneo yao hata kama
hawajui katiba iliyopita kwa kuwa maoni hayo si lazima yatokane na katiba ya
sasa bali kuangalia changamoto katika maeneo wanayoishi.
Bi Mwatum Malale ambaye ni mjumbe wa tume ya mabadiliko ya
katiba ameyasema hayo alipokuwa akiongea na radio kwizera na kuongeza kuwa ni
vema wananchi wakijitokeza kwa wingi katika kuchangia katiba hiyo kwa kuwa ni
suala la kihistoria linalojitokeza mara moja baada ya miaka mingi
Bi Malele pamoja na mambo mengine ameshauri akina mama kutoa
michango yao na si kutazama tu wengine wakichangia maoni kwenye katiba ya nchi
hii kwa kuwa ni suala la kihistoria ambalo huja mara moja baada ya muda mlefu
na kwamba maoni yote yatakayotolewa yatafanyiwa kazi bila kujali kama
yanapatikana katika katiba ya sasa
Bi malale amewataka wananchi kusema mambo wanayohisi
yanaweza kuingia kwenye katiba kwa kuwa yanaweza kusaidia katika kuandika
katiba mpya kutokana na kuwa tume hiyo itafahamu kwa undani ni mambo gani
wananchi hawapendi na mambo wanayopenda
Tume ya mabadiliko ya katiba kwa hivi sasa iko mkoani kigoma
ambapo hii leo imeanza kukusanya maoni katika kata za wilaya ya kakonko ambapo
tarehe 31 agost mpaka tarehe 3 septemba watakuwa katika kata za wilaya ya
kibondo MWISHO
No comments:
Post a Comment