Pages

Friday, August 31, 2012

watu watatu watekwa kanembwa na kupigwa risasi

bw josephat maimu aliyejeruhiwa katika mateka yaliyofanywa na majambazi katika poli la kanembwa akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya kibondo  (picha na james jovin)

KIBONDO
watu watatu wamejeruhiwa kwa kupigwa na lisasi baada ya kutekwa na watu wasiojulikana katika poli la kanembwa wilayani kibondo mkoani kigoma na wawili kati yao wamelazwa katika hospital ya wilaya ya kibondo

watu hao ni pamoja na bw Josephat Maimu 31 , Shukuru Benet 25 na Noel godifrey 21 na walikuwa wakisafiri kuelekea kahama katika shughuli zao za kawaida

mmoja wa majeruhi hao bw Josephat Maimu ameelezea jinsi tukio hilo lilivyotokea na kwamba kabla ya tukio hilo kutokea aliona magari mawili yakiwa yamesimama akidhania kuwa walikuwa wamepata pancha

muuguzi wa zamu katika hospital ya wilaya ya kibondo bi Christina Samizi amesema kuwa hali ya majeruhi sio mbaya na kwamba wanaendelea na matibabu  MWISHO


bw josephat maimu akiwa katika hospitali ya wilaya kibondo baada ya kujeruhiwa na majambazi katika poli la kanembwa kibondo (picha na james jovin)

No comments:

Post a Comment