KIBONDO
Mtoto mwenye umri wa miaka mitano amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari la polisi wilayani kibondo mkoani kigoma lenye namba za usajili PT 1817
Tukio hilo limetokea hapo leo novemba 6 majira ya asubuhi katika eneo lililoko karibu na Benk ya NMB wilayani hapa na jeshi la polisi limemtaja mtoto huyo kuwa ni Nasibu Salum mwenye umri wa miaka mitano
Aidha chanzo cha ajali hiyo ni kwamba mtoto huyo alikuwa akivuka bara bara kwenda kwenda kununua vitumbua ndipo akagongwa na gari hilo la polisi lililokuwa likiendeshwa kwa mwendo kasi na askari PC Ruben amabaye ni dereva wa gari hilo
Baada ya kutokea kwa ajali hiyo wananchi walikataa kutoa maiti hiyo barabaran i wakidai kuwa gari lililomgonga ndilo linapaswa kutoa maiti hiyo ndipo mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto akalazimika kuja kutoa maiti hiyo barabarani kwa kutumia gari lake binafsi na kuipeleka maiti hiyo hospitali ya wilaya
Jeshi la polisi wilayani hapa limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba dereva huyo aliamua kujisalimisha kituo cha polisi baada ya kutokea kwa tukio hilo MWISHO
No comments:
Post a Comment