Jeshi la polisi wilayani kibondo mkoani kigoma limekamata siraha moja aina ya SMG na lisasi 10 vikiwa vimefukiwa ardhini nyuma ya nyumba ya mkazi wa kata ya Busunzu baada ya kupata taarifa za siri kutoka kwa raia wema
Taarifa zinasema kuwa siraha hiyo imekamatwa juzi novemba 6 mwaka huu na OCS wa kituo cha polisi kifura pamoja na askari wenzake waliokuwa doria na kwamba ilikuwa imechimbiwa ardhini nyuma ya nyumba ya bw Ntamundu Kachukuzi mkazi wa kata ya busunzu
Aidha jeshi la polisi limesema kuwa siraha hiyo ilikuwa na namba UG 4872 – 1998 na kwamba bw Kachukuzi baada ya kupata taarifa kuwa polisi walikuwa nyumbani alitoroka ambapo mbaka hivi sasa bado hajapatikana na jeshi hilo linaendelea kumtafuta
Jeshi la polisi limetoa wito kwa raia wanaomiliki siraha kinyume cha sheria kuzisalimisha katika vituo vya jeshi hilo kwa wakati huu ambao limeanzisha mpango wa kusalimisha siraha kwa hiari na kwamba ifikapo decemba 2 mwaka huu msako mkali utafanyika na atakae kutwa na siraha atachukuliwa hatua za kisheria MWISHO
No comments:
Post a Comment