Pages

Wednesday, January 23, 2013

diwani kata ya Busagara pamoja na afisa mtendaji washitakiwa kwa kosa la kufyeka mazao ya mkulima




Viongozi wa wiwili wa serikali wilayani Kibondo mkoani kigoma wamefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma za kuharibu mazao yenye thamani ya shilingi laki tano na elfu hamsini

Mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya bw Erick Marley Mwendesha mashitaka wa polisi bw Fadhil Noel Tambale amewataja viongozi hao kuwa ni diwani wa kata ya Busagara bw Godwin Robert Sibanilo mwenye umri wa miaka 49 pamoja na afisa mtendaji wa kata hiyo bw Baruan Gwimo mwenye umri wa miaka 34

Aidha bw Tambale amesema kuwa tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Kasaka kilichoko kata ya Busagara mnamo January 10 mwaka huu majira ya saa mbili za asubuhi kinyume na sheria za nchi viongozi hao walifyeka mazao ya bw Kobantinda Jankisi mkazi wa kijiji cha Kasaka wakidai kuwa eneo hilo ni la kujenga ofisi za kijijij

Bw Tambale amesema kuwa mwaka 2005 viongozi wa serikali ya kijiji cha Kasaka walionywa na wakili wa serikali wakati huo bw Balichako M N kutofanya shughuli zozote za kijiji katika kiwanja hicho endapo hawawezi kulipa fidia kwa mmiliki wa kiwanja hicho

Hakimu wa mahakama ya wilaya bw Erick Marley  ameahilisha shauri hilo baada ya viongozi wote wawili kukana tuhuma hizo  mpaka litakapotajwa tena Februay 07 mwaka huu kwa ajili kuachia nafasi jeshi la polisi  kukamilisha upelelezi wa shauri hilo MWISHO

No comments:

Post a Comment