kijana susuruka akiwa hospitali ya wilaya ya kibondo |
KIBONDO
Kijana aliyefikishwa katika hospitali ya wilaya ya kibondo baada ya kung,atwa sehemu kubwa ya uso na mwajiri wake anaendelea kupata matibabu na mikakati ya kumkabidhi kwa uongozi wan chi jirani ya Burundi umeanza kupitia ofisi ya mganga mkuu wa wilaya baada ya kubainika kuwa ni raia wa nchi hiyo
Akiongea na kibondo moto mganga wa wodi ya wagonjwa majeruhi Dr Victor Nzaro amesema kuwa hali ya kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Susuruka inaendelea vizuri na kidonga kilichoko usoni kiko kwenye hatua za mwisho kupona
Aidha Dr Nzaro amesema kuwa kijana huyo aliyekumbwa na tukio hilo katika kijiji cha Muhange ya juu sio raia wa Tanzania hivyo mipango inafanyika ili kumrudisha nchini kwao Burundi alikotokea ambapo alifika nchini tanzania kwa ajili ya kutafuta kazi ya kuweza kukidhi mahitaji yake
Dr Nzaro ameitaka jamii kumpokea vizuri kijana huyo na kuelewa kuwa tayari amekuwa mlemavu baada ya kupoteza viungo vyake kama masikio, macho , pua na mdomo wa juu na chini hali inayopelekea kutokuwa na uwezo wa kujitafutia chakula
Mipango ya kumrejesha nchini kwao itategemeana na makubaliano kati ya Tanzania kupitia mambo ya ndani kwa kushirikiana na uhamiaji pamoja na uongozi wa nchi ya Burundi MWISHO
hujafa hujaumbika lolote laweza kutokea ukiwa bado unaishi na unaweza kudhani ni hadith lakini ni mambo ambayo yanatokea duniani |
No comments:
Post a Comment