Pages

Wednesday, March 13, 2013

wilaya ya kibondo kutumia bilioni 33 katika mwaka wa fedha 2013/2014

Halimashauri ya wilaya ya kibondo imepanga kukusanya na kutumia kiasi chaShilingi billion 35 milioni 182 tisini na tisa eluf na mia tisa ishirini katika mwakaWa fedha 2013/2014

Akiongea katika mkutano maarumu wa kujadili na kupitisha bajeti ya mwaka Wa fedha 2013/2014 afisa mipango wa halmashauri bw Wilbard Bandola Amesema kuwa fedha hizo zitatoka katika ruzuku ya serikali kuu , mapato Ya ndani na michango ya wahisani wa maendeleo

Aidha Bw Bandola amesema kuwa serikali kuu imeombwa kuchangia bilioni 33 Milioni 876 mia nne na moja elfu ikiwa ni pamoja na fidia ya kodi zilizofutwa Kiasi cha shilingi milion 233 laki 5 na elfu 15

Bw Bandola amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya kibondo imeanza Kuangalia njia bora ya kuinua kipato chake cha ndani kwani kwa sasa Inategemea serikali kuu kwa zaidi ya asilimia 96
kuanzia kushoto mkuu wa wilaya ya kibondo Venance mwamoto mwenyekiti wa halmashauri bw Juma Maganga na mkuu mkurugenzi wa halamashauri bw Leopord Ulaya katika kikao maarumu cha madiwani

mkurugenzi mtendaji Leopord Chudu Ulaya akisisitiza jambo katika baraza la madiwani lililoketi 11march 2013



 aidha Halimashauri ya wilaya ya kibondo inakusudia kutumia fedha za maendeleo kiasi cha shilingi bilioni 10 milioni 600 mia nne thelathini na sita elfu na mia tatu sitini na tatu kwa ajili ya kupunguza au kumaliza baadhi ya vikwazo vinavyoathili kuboreshwa kwa huduma za kijamii na kukua kwa uchumi

Ameyasema hayo afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya kibondo bw Wilbard Bandola wakati akisoma mapendekezo ya mipango na bajeti ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2013/2014 bajeti ambayo tayari imepitishwa na baraza la madiwani wilayani humo

Aidha Bw Bandola amesema kuwa fedha nyingi zimeelekezwa katika kukamilisha  miradi vipolo hasa ile ilivyoko katika maeneo ya vijijini ili kuvutia maeneo hayo kwa watumishi wapya wanaoajiriwa hali itakayosaidia kuinua utoaji wa huduma za jamii kama vile elimu na huduma za afya

Bw Bandola amesema kuwa sekta ya elimu ya msingi , elimu ya sekondari  sekta ya afya , maji ,kilimo na barabara zimepewa kapaumbele lengo likiwa ni kuchochea maendeleo na kukuza uchumi wa watu wa vijijini ambayo ni asilimia 85 ya wakazi wa halmashauri ya wilaya ya kibondo MWISHO


No comments:

Post a Comment