Pages

Thursday, June 6, 2013

utekelezaji wa irani ccm katika kata ya Busagara



KIBONDO

Zaidi ya shilingi milioni 240 zimetolewa na serikali  katika utekelezaji wa miradi mbali mbali katika sekta ya afya elimu kilimo na utawala ikiwa ni utekelezaji wa irani ya uchaguzi ya mwaka 2010


Ameyasema hayo afisa mtendaji wa kata ya Busagara bw Baruan Gwimo wakati akisoma lisara mbele ya mgeni lasmi Mwenyekiti waccm bw Emmanuel Gwegenyeza alipotembelea kata hiyo kwa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa irani


Pamoja na mambo mengine bw Gwimo ameitaka serikali kuelekeza miradi ya maji katika kata hiyo kwa kuwa tangu mwaka 2010 hakuna mradi wowote wa maji uliotolewa katika kata hiyo


Kwa upande wake mgeni lasmi na mwenyekiti wa ccm wilaya ya Kibondo bw Emanuel Gwegenyeza amepongeza utekelezaji wa miradi hiyo ya elimu afya na kilimo na kuongeza kuwa ataweka msukumo ili serikali ipeleke miradi ya maji katika kata hiyo Ends

No comments:

Post a Comment