Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine kumi na
tatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata pancha ya taili ya
nyuma kisha kuanguka eneo la
kazilamihunda kakonko kutokana na mwendo kasi wa gari hilo lililokuwa likitokea
nyakanazi kwenda kibondo
Jeshi la polisi wilayani kakonko limesema kuwa waliouwawa ni
mwanaume mmoja pamoja na mwanamke mmoja ambao hawakujulikana majina yao mara
moja na miili yao iko katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya
kakonko
Aidha jeshi hilo limebainisha kuwa dereva wa gari hilo bw
adrof sadock ametoroka baada ya kutokea kwa ajali hiyo na mpaka sasa hajulikani
aliko
Baada ya kutokea kwa ajali hiyo basi moja ambalo lilikuwa
nyuma ya gari hiyo iliyopata ajali liliwachukua majeruhi wote na kuwakimbiza katika
hospitali ya wilaya ya kibondo kwa matibabu Zaidi
Mganga mfawidtdh wa hospitali ya wilaya ya kibondo dr
frolian tinuga amekili kupokea majeruhi hao 13 na kwamba hali zao zinaendelea
vizuri na wanaendelea na matibabu
Baadhi ya majeruhi waliokuwemo katika gari hilo wameelezea
chanzo cha ajali hiyo wakisema kuwa ni mwendo kasi na kwamba taili la nyuma
lilipata pancha hivyo gari liliyumba sana na kusababisha kuanguka na kubinuka
mara kadhaaa
Jeshi la polisi wilaya ya kakonko limethibitisha kutokea kwa
ajali hiyo na kwamba ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota hiace lenye
namba za usajili T 498 csm na kwamba upelelezi Zaidi wa tukio hilo bado
unaendelea
No comments:
Post a Comment