Pages

Sunday, December 16, 2012

mbunge wa jimbo la muhambwe afanya mkutano kupinga tuhuma mbali mbali alizotuhumiwa kwenye mkutano wa ccm akumbana na vikwazo vya mabango kama kawaida

mbunge wa jimbo jla muhambwe mh. Felix Mkosamali akihutubia wananchi wa jimbo hilo na kufafanua kuwa watu wanaouza bidhaa ndogo ndogo hawapaswi kutoza ushuru

mbunge wa jimbo la muhambwe  wilayani kibondo mkoani kigomabw Felix Mkosamali kushoto na Katibu wake bw Vedasto Pesambili wakisikiliza maswali kutoka kwa wananchi

mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kibondo bw Juma Maganga alikuwepo kwenye mkutano huo wa hadhala yeye pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa ni lazima wananchi watoe ushuru kwa maendeleo yao

haya nayo ni mabango yaliyowekwa na wananchi wakipinga falasfa za mbunge huyo yaone halafu utajua mwenyewe yana maanisha nini







mamia ya wananchi walihudhulia mkutano huo kusikiliza sera za mbunge wao
katika mkutano wake mbunge huyo bw Mkosamali amesisitiza kuwa wafanya biashara wanaopaswa kutozwa ushuru ni wale ambao ni walanguzi na kwamba wafanya biashara wadogo wadogo hawapaswi kutozwa kodi kwa kuwa tayari swala hilo limeongelewa bungeni

aidha amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya kibondo inaweza kukusanya mapato katika vyanzo vyake vikubwa kama nyumba za kulala wageni jengo la vijana pamoja na baa marufu kama KIBODECO kuliko kulazimisha wananchi wadogo kuoa ushuru ambao hauwezi kukidhi matakwa ya wana kibondo kwa ujumla

1 comment:

  1. Sasa hayo mabango yote mbona kama yameandikwa na mtu mmoja?

    ReplyDelete