Mshambulaji wa Liverpool Mario
Balotelli, ameomba radhi kwa kuweka picha yenye kuashiria vitendo vya
kibaguzi katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram. Balotelli 24,
mwenye matukio mengi ya utukutu, haraka alifuta picha hiyo iliyokuwa
kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“naomba radhi kwa yoyote aliekwazika. Nilifikiri kuwa ilikua ni ucheshi na sio ubaguzi ,sikujua kama inaweza kuwa na athari”.Sakata hili la Balotelli limempelekea kocha wa Arsenal Wenger kuzungumza na kusema wachezaji wanapaswa kujichunga kwa kile wanachoweka kwenye mitandao ya kijamii
“Tunaweza kuwachunga na hatari ila hatuwezi kuwachunga wachezaji saa 24 za siku,wanawajibu wa kujichunga na nakuwa makini kwa kile wanachoandika”.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester City na Ac Milan alikosa mchezo ligi dhidi ya Leicester City sababu ni majeruhi.
No comments:
Post a Comment