Add caption |
chanzo mwananchi
Dar es Salaam. Wakati Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ukitarajiwa
kufanyika kesho nchi nzima, wafuasi wa (Chadema) na Jeshi la Polisi,
wamekamata karatasi zinazodaiwa za kupigia kura kwenye uchaguzi huo za
Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, zikirudufiwa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Jimbo la Ubungo,
Justine Mollel, tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati mwanachama wa chama hicho alipokwenda katika duka la vifaa vya shule na ofisini saa 8 mchana kwa lengo la kurudufu karatasi za chama hicho lakini aliambiwa arudi saa 12 jioni.
Justine Mollel, tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati mwanachama wa chama hicho alipokwenda katika duka la vifaa vya shule na ofisini saa 8 mchana kwa lengo la kurudufu karatasi za chama hicho lakini aliambiwa arudi saa 12 jioni.
Gazeti hili lilifanikiwa kuiona moja ya nakala
hizo kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ikiwa na nembo ya Halmashauri ya
Wilaya ya Kilosa, ikiwa na nafasi ya kupigia kura kwa wagombea wa CCM
na Chadema.
abari zaidi zinaeleza kuwa tayari zaidi ya nakala milioni moja zilisharudufiwa, huku zikiwa zimewekwa alama ya ndiyo kwa mmoja wa wagombea wa vyama hivyo.
abari zaidi zinaeleza kuwa tayari zaidi ya nakala milioni moja zilisharudufiwa, huku zikiwa zimewekwa alama ya ndiyo kwa mmoja wa wagombea wa vyama hivyo.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Camillius
Wambura alisema: “Uchunguzi bado unaendelea kwani waliokuwa wanarudufu
walijitambulisha kuwa ni wasimamizi wa uchaguzi, hivyo tunaendelea na
uchunguzi na hakuna mtu tunayemshikilia.”
Aliongeza: “Nimemwagiza OCD (Mkuu wa Polisi wa
Wilaya) kuwasiliana na Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa)
ili kujua hizo karatasi ni kweli zilitakiwa kutengenezwa hapo au la...
Kama ni hapo mambo yaishie palepale na kama siyo halali basi hatua
zichukuliwe kwa wahusika.”
Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu
Tamisemi, Khalist Luanda alisema kurudufu karatasi za kupigia kura
kunatakiwa kufanyika katika wilaya au mkoa lakini siyo nje ya mkoa.
“Ni kosa kuchapa fomu za wagombea kutoka wilaya
moja kwenda nyingine walipaswa kurudufu katika eneo kunapofanyika
uchaguzi au wilaya husika na mchakato unaopaswa kuwa wa siri sana na
siyo kila sehemu kwani haitakuwa rahisi kusafirisha kwa usalama bila
kutiliwa shaka.”
Aliongeza kuwa: “Nimesikia katika vyombo vya
habari na nimetuma wataalamu wangu kwenda kufuatilia jambo hilo kwani ni
makosa na mkurugenzi huyo inaonyesha alikuwa na malengo au masilahi
binafsi na kama ni kweli anatakiwa kuwajibika.”
Awali akisimulia tukio hilo Mollel alisema:
MwanaChadema alikwenda pale kurudufu karatasi zake kwani gharama yake ni
Sh25 kwa karatasi moja na aliambiwa arudi jioni kwani walikuwa na kazi
maalumu, hivyo wasingeweza kumrudufia karatasi zake.”
Aliongeza: “Alipokwenda tena saa 12 aliambiwa bado
hawajamaliza kazi hiyo maalumu hapo alipata hofu na kuanza kuchunguza
kazi iliyokuwa ikifanyika, ndipo alipoona karatasi za kupigia kura
zikirudufiwa.”
Mollel alifafanua kuwa alipoona hivyo mfuasi huyo
aliwaita wanachama wengine wa Chadema waliozingira duka hilo lililopo
maeneo ya Mabibo kabla ya kutoa taarifa Kituo cha Polisi Mabibo umbali
wa takriban mita 100.
Alisema polisi wa Mabibo na baadaye wa Magomeni walipofika
waliwachukua wahusika na kuwapeleka Kituo cha Polisi Magomeni kwa ajili
ya kuandika maelezo.
Shuhuda ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema:
“Niliingia dukani hapo nikakuta wanachapisha hizo karatasi, lakini
sikujali sana kwani nilikuwa nina haraka zangu, lakini baadaye
niliporudi nikakuta baadhi ya hizo nyaraka zikiwa mezani na ndipo
nikagundua kuwa ni nyaraka za siri ambazo hazitakiwi kuonekana kwa muda
huo.”
Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Saidi Meck Sadiki alisema maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo
yamekamilika kwa vifaa vyote kufika katika maeneo yatakayotumika kwa
uchaguzi huo.
Alisema jumla ya wenyeviti wa mitaa 559 na wajumbe
2,795 wanatarajiwa kuchaguliwa. Jumla ya vituo 1,674 vya kupigia kura
vitatumika huku masanduku yakiwa 5,022 na karatasi za kupigia kura
zikiwa 1.7 milioni.
“Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2 asubuhi hadi
saa 10 jioni, tunawaomba wananchi waliojiandikisha wajitokeze kupiga
kura lakini wazingatie taratibu na sheria za uchaguzi,” alisema Sadiki.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova alisema, “Kila chama kihakikishe hakivunji sheria kwani
hatutakuwa na hiana na mtu yeyote, ukienda kinyume tutakuchukulia hatua
kali bila kujali chama ulicho na wadhifa wako.”
Aliongeza: “Tunawaomba wanawake ambao mara nyingi
wamekuwa waoga kwenda kupiga kura wakihofia usalama wao kujitokeza kwa
wingi kwani tumejipanga vizuri kiulinzi kuhakikisha uchaguzi unaanza na
kumalizika salama.”
usikose kutembelea blog yako kibondo moto kwa habari moto moto kila siku
No comments:
Post a Comment