sala ya mwisho marehemu Issa Ngumba |
Vyama vya siasa wilayani kibondo mkoani kigoma vimetoa
salamu za lambi lambi kwa familia pamoja na wafanya kazi wote wa radio kwizera
kufuatia kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa radio kwizera issa ngumba
aliyeuwawa mwanzoni mwa wiki hii na watu wasio fahamika
Kwa niaba ya wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya
kibondo na kakonko katibu wa chama hicho bw Kisali Elia ametoa salamu hizo za
lambi lambi na kuongeza kuwa chama kimepokea kwa masikitoko taarifa hiyo ya
mauaji
Aidha bw Elia amesema kuwa chama cha mapinduzi kitamuenzi bw
Issa Ngumba kwa kuendeleza utekelezaji wa kauli yake aliyoitoa katika moja ya
habari zake ya kuwaasa wanachama kujitokeza kwenye vikao vya chama
Bw Elia amesema kuwa chama cha mapinduzi hakiungi mkono
tabia ya wananchi ya kujichukulia sheria mkononi na kwamba ni vyema wananchi
wakaamini vyombo vya dola na kuvitumia pale wanapokuwa wamebaini makosa yoyote
badala ya kuchukua maamuzi ambayo huleta athali kubwa kwa jamii
Aidha Chama cha wananchi CUF wilayani Kibondo mkoani kigoma
kimewataka wananchi wilayani kakonko kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi
na kutoa taarifa za kweli wakati huu ambapo jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa tukio la
kuuwawa kwa mwandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii
Katibu wa chama hicho bw Vedasto Pesambili ameiambia kibondo
moto kuwa wananchi wanapaswa kuwa wazalendo na kutoa taarifa sahihi ili
kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo ambali bado lina utata
Aidha pamoja na mambo mengine bw Pesambili ameomba wananchi
kutoa taarifa ambazo ni sahihi na kuepuka kusingizia raia wasio na hatia
kutokana na visa ambavyo havihusiani na tukio hilo
Bw pesambili ametoa wito pia kwa wananchi kutojichukulia
sheria mkononi bali kuacha sheria ichukue mkondo wake akiwataka pia polisi
kutotumia nguvu nyingi katika kudhibiti uhalifu
Mwandishi wa habari wa radio kwizera issa ngumba ambaye ni mkazi wa wilaya ya kakonko aliuwawa
na watu wasiofahamika mwanzoni mwa wiki hii katika poli la Kudayamuheta lililopo katika kijiji na
kwamba jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi wa kifo hicho kilichokuwa
na utata
No comments:
Post a Comment