Wakaazi wa Kismayo waliwaambia waandishi wa habari kwamba wapiganaji hao waliondoka usiku na kwamba mji sasa ni shuwari.
Majeshi ya Kenya na serikali ya Somalia, ambao
walikuwa wakipigana na Al Shebaab kilomita kadha nje ya mji hapo jana,
bado hawakuingia mjini.
Kismayo ni bandari ya pili ya Somalia kwa ukubwa na ikileta pato muhimu kwa al-Shabaab.
Wakaazi wa Kismayo wanasema waliamka leo asubuhi na kukuta Al Shebaab wameshaondoka.
Kwenye ukurasa wao wa mtandao wa internet wa
twitter, kundi la al-Shabaab limetoa tangazo hili: "jana usiku, baada ya
miaka mitano, utawala wa Kiislamu mjini Kismayo ulifunga ofisi zake".
Wanajeshi wa Kenya na serikali ya Somalia bado hawakuingia ndani ya mji.
Msemaji wa jeshi la Kenya aliiambia BBC kwamba ana wasiwasi kuwa kuondoka kwa al-Shabaab pengine ni mtego.
Kwa hivo kwa sasa, Kismayo haidhibitiwi na mtu yoyote.
Yote yanategemea vipi serikali ya Somalia na
washirika wao wa Umoja wa Afrika watavosarifu maslahi yao yanayogongana,
kudhibiti mji huo wenye bandari na unaoleta pato.