Pages

Sunday, September 30, 2012

Bajeti ya Ufaransa kukabiliana na deni

Waziri mkuu nchini Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, ameitaja bajeti ya serikali yake ya mwaka 2013 kama silaha dhidi ya madeni ya nchi hiyo yanayo ongezeka kila kukicha.

Huku deni la nchi hiyo likikadiriwa kuwa asilimia tisini ya mapato ya nchi hiyo, bwana Ayrault alisema kuwa bajeti hiyo itajumuisha kuongezwa kwa kodi kwa watu wanaopokea mishahara mikubwa.

Tisa kati ya watu kumi hata hivyo hawataathirika kutokana na kupandishwa kwa viwango vya kodi.
Mpango huo wa serikali unasemekana utaweza kuchangisha dola bilioni ishirini na sita kwa pesa za serikali na kuzuia mipango ya kupunguza matumizi ya pesa za umma ambayo imeathiri nchi nyingi Ulaya.

Alisema kuwa serikali itahakikisha imetumia pesa kulingana na mahitaji ya nchi , yale muhimu yakipewa kipaombele kama elimu, ukosefu wa ajira , usalama na haki.
Katika wiki moja iliyopita, kiwango cha ukosefu wa ajira kimefika zaidi ya watu milioni tatu.

No comments:

Post a Comment