Serikali wilaayani kibondo mkoani kigoma imewataka viongozi
wa ngazi zote katika vijiji na kata kuhakikisha wanakuwa makini na kutoa elimu
kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutoa taarifa mapema pale watakapogundua mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola
Maagizo hayo kwa viongozi wa vijiji na kata yametolewa na
katibu tawala wa wilaya ya kibondo bw Ayubu Sebabili wakati wa maadhimisho ya
wiki ya elimu yaliyofanyika katika kata ya misezero hapo juzi August 26 ambapo
alialikwa kama mgeni lasmi katika maadhimisho hayo
BW Sebabili amesema kuwa ni vema wananchi wakawa makini hasa
ukizingatia kuwa wilaya ya kibondo ipo mpakani na tayari nchi jirani ya congo
DRC imetangaza uwepo wa wagonjwa wa ebola katika nchi hiyo hivyo kuna uwezekano
mkubwa wa watu kusafiri na ugonjwa huo hasa mipakani
Amesema viongozi wa vijiji na kata wanapaswa kuwa makini na
kuelimisha wananchi juu ya ugonjwa wa ebola ikiwa ni pamoja na kuwapeleka
wagonjwa wote wenye dalili za ugonjwa wa ebola katika zahanati iliyo karibu au
kituo cha afya ili waweze kuchunguzwa na kupewa rufaa ya kwenda katika
hospitali kubwa iwapo watakutwa na dalili au maambukizi ya ugonjwa huo
Bw Sebabili amesema kuwa kwa mjibu wa wizara ya afya dalili
za ugonjwa wa Ebola ni pamoja na homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya
misuli, kuuma kichwa, na vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na
kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na
kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje mwilini.ENDS
No comments:
Post a Comment