KIBONDO
Mkazi wa kijiji cha Bukirilo wilayani Kibondo mkoani kigoma
amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo baada ya kujeruhiwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbali mbali za
mwili wake
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dr Frolian Tinuga amesema
kuwa amempokea mgonjwa huyo ambaye amejulikana kwa jina la Bi Ester Ntikahela mwenye umri wa miaka 40 na
kwamba hali yake inaendelea vizuri
Dr Tinuga amesema kuwa baada ya kumpokea mgonjwa huyo
amepatiwa huduma ya kwanza kwa kumushona katika majeraha hayo ambayo yako
katika sehemu mbali mbali za mwili wake pamoja na matibabu mengine ya muhimu
Bi Ntikahela amesema kuwa kitendo hicho cha ukatili
kilifanywa na mtu aliyekuwa akimdai pesa shilingi miliono moja na alifanya
hivyo baada ya kuona kuwa asingepata hela za kulipa deni hilo MWISHO
hhh
No comments:
Post a Comment