KIBONDO.
Idara ya Afya ya halmashauri ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imeshindwa kufikia malengo ya kuboresha huduma za afya kutokana na idadi ndogo ya kaya zinazochangia mfuko wa afya ya jamii CHF.
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Kibondo Bw. Emmanuel Mwasulama amesema kutokana na ufinyu wa bajeti katika idara za afya pamoja na uchangiaji usio lidhisha wa jamii wameshindwa kupata dawa za kutosha, vitendanishi pamoja na vifaa tiba vinavyoweza kukidhi mahitaji ya wakazi wa kibondo.
Dr. Mwasulama amesema mpaka sasa asilimia 17% pekee ndio wamechangia CHF sawa na kaya 13,041 kati ya kaya 74,508 kwa kata moja ya kitahana, ikiwa na idadi ndogo sana ukilinganisha na idadi ya kaya zote katika tano za wilaya ya kibondo.
Aidha ametoa wito kwa wakazi wa wilaya ya kibondo kujitokeza ili kuchangia mfuko wa afya ya jamii ili kupunguza tatizo la upatikanaji wa dawa katika Zahanati na vituo vya afya kwani fedha hizo ziweze kuongeza kiwango cha dawa, vifaa tiba.End’s
No comments:
Post a Comment