Pages

Friday, December 7, 2012

viongozi wa ccm mkoa wa kigoma wamvalia njuga mbunge wa jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo

Dr. Walid Amani Kabourou mwenyekiti wa ccm mkoa wa Kigoma
Viongozi wa ccm mkoa wa kigoma wamefanya ziara wilayani kibondo ikiwa ni miezi takribani  miwili tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho katika ziara hiyo wamekagua utekelezaji wa miradi mbali mbali ikiwa ni utekelezaji wa irani ya chama

Baada ya ukaguzi huo wa miradi mbali mbali walifanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa vijana maarufu kama community center ulioko mjini kibondo ambapo pamoja na mambo mengie  wamemtaka mbunge wa jimbo la muhambwe wilayani kibondo mkoani kigoma bw Felix Mkosamali kuacha tabia ya kushinikiza  wananchi kutochangia miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuacha kukashifu viongozi wa serikali  


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kigoma bw Walid Amani Kabourou amesema kuwa kitendo cha mbunge wa jimbo la muhambwe bw Felix Mkosamali kumtukana mkuu wa wilaya hiyo pamoja na kuzuia shughuli za maendeleo kufanyika wilayani humo si jambo jema kwa maendeleo


Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa kigoma bw Mohamed Nyawenga amesema kuwa hasira ya mkizi ndio iliyowaponza wananchiwa wilaya ya Kibondo kwa kuchagua kiongozi ambaye hafai


Aidha mwenyekiti wa ccm wilaya ya Kibondo bw Emmanuel Gwegenyeza amemtaka mbunge huyo kufanya shughuli za maendeleo ya wananchi waliomchagua na si kutafuta umaarufu na kutumia muda mwingi kukashifu viongozi wengine kwa mambo yasiyo ya msingi

Katibu mwenezi ccm mkoa bw kalembe masoud king’ombe nae hakubaki nyuma na alipata nafasi ya kutoa machache juu ya mbunge wa jimbo la muhambwe bw Felix mkosamali ambapo amesema kuwa hasira za wananchi wa kibondo ndizo zilizosababisha wachague kiongozi ambaye hafai kutokana na kwamba waliona kuliko kumchagua bw Jamal Tamimu ni bora wachague bw mkosamali

Aidha mbunge wa jimbo la muhambwe wilayani kibondo bw Felix mkosamali baada ya kusikia shutuma hizo amesema kuwa atafanya mkutano wa hadhara Jumamosi ya December 15 mwaka huu ili kujibu baadhi ya tuhuma hizo ambazo amesema kuwa ni propaganda za kisiasa

Siku za hivi karibuni mbunge wa jimbo la muhambwe bw Felix Mkosamali alishutumiwa kwa vitendo vya kuwakataza wananchi kutoa ushuru ,kuwakataza wananchi wa kijiji cha Mkalazi kuchangia ujenzi wa choo cha shule ya msingi , kushinikiza wananchi kuwakataa wenye viti wa vijiji pamoja na kugawa mashamba ya wananchi katika kataya Mabamba  MWISHO

viongozi wa ccm mkoa wa kigoma wakifanya mkutano wa hadhara wilayani kibondo

No comments:

Post a Comment