Wananchi wilayani kibondo wametakiwa kutoa maoni yatakayosaidia kuandikwa kwa katiba mpya itakayoiongoza Tanzania kwa miaka mingine zaidi ya 50 na si kutoa malalamiko ya matatizo yaliyoko kwenye jamii ambayo hayana maana katika uandikaji wa katiba
Ameyasema hayo mwezeshaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali bw Ramadhan Joel wakati wa mdaharo ulioandaliwa na muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilayani kibondo KINGONET uliofanyika katika ukumbi wa vijana ulioko kibondo mjini
Aidha bw Joel amesema kuwa ni vema wananchi wakazungumzia mambo mbali mbali ambayo ni muhimu katika uandikaji wa katiba na kwamba katiba hiyo ndiyo msingi wa maisha yetu ya kila siku ambapo binadamu popote pale anapoishi ni lazima aishi kwa mwongozo
Kwa upande wake mwenyekiti wa KINGONET bw Julius Nuba amesema kuwa muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilayani hapa wameamua kuandaa mdaharo huo kwa ajili ya wananchi kutoa maoni yao ikiwa ni kwa wale ambao hawakupata nafasi wakati tume huru ya kukusanya maoni ilipopita wilayani hapa mwanzoni mwa mwezi Augost
Bw Nuba ameendelea kwa kusemaa kuwa baada ya kukusanya maoni hayo katika awamu nnne katika maeneo tofauti yatapelekwa kwenye tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya kwa ajili ya kufanyiwa kazi na kwamba wananchi wasiwe na wasi wasi juu ya maoni wanayoyatoa na alisema kuwa katiba iliyopo ina zaidi ya miaka 50 hivyo ilikuwa inafaa kwa wakati ule kwa kwakuwa ilikuwa ni maoni ya watu wachache nasasa inatakiwa katiba ya watanzania wote pia inayokwenda na wakati
Kwa upande wake Bw Emmanuel koreshi ambaye ni mwananchi wakawaida alipokuwa akitoa maoni yake alisema kuwa yeye anawasiwasi na tume ya kuratibu na kukusanya maoni iliteuliwa na Rais na watu wengi wanatoa maoni mengi yanayomzungumzia yeye tena kwa kulalamikia mamlaka yake hivyo watendaji wa Tume hiyo hawawezi kueleza sawasawa wasije wakamkorofisha Bosi wao
Kwa upande mwingine Kwakuwa kuna nchi ambazo zinaomba kujiunga na jumuhiya ya Afrika ya masharikiki, ambazo katiba zao zinaongozwa naserkali za kidini na Katiba ya nchi yetu inasema serikali yetu haina Dini basi katika katiba tuitakayo kiwepo kipengele cha kukataa kujiunga na nchi zenye mfumu huo
No comments:
Post a Comment