Pages

Friday, September 14, 2012

zahanati wilayani kibondo zakabiliwa na tatizo la maji

KIBONDO
Baadhi ya zahanati wilayani kibondo mkoani kigoma zinakabiliwa na tatizo la maji kitu kinachopelekea wagonjwa kulazimka kwenda na lita tatu za maji katika zahanati hizo  ili waweze kupata huduma ya matibabu

Akiongea na waandishi wa habari muuguzi katika zahanati ya kijijij cha bitale bi Joyce Mihungo amesema kuwa tatizo la maji katika zahanati hiyo limekuwepo kwa muda mlefu kiasi ambacho tayari wananchi wameshazoe kuja na maji katika zahanati hiyo pindi wanapokuwa wameugua

Bi Mihungo amesema kuwa mara nyingine hulazimika kutafuta maji yeye mwenyewe ili kuweza kuwahudumia wagonjwa ambao hawakuweza kufika na maji ambayo ni muhimu katika huduma mbali mbali katika kuhudumia wagonjwa

Amesema kuwa tatizo hilo la maji limetokana na kuhalibika kwa vifaa katika kisima ambacho pia wakazi wa kijiji cha bitale wanakitegemea kwa kiasi kikubwa   na kwamba  tayari wagonjwa wanaofika hospitalini hapo wamezoea kuja na maji kwa kuwa wauguzi wa zahanati hiyo pamoja na viongozi wa kijiji walitangazia wananchi kuwa ni lazima wafike na maji lita tatu ili kupatiwa huduma ya matibabu

Aidha bi Mihungo ameiomba halmashauri ya wilaya ya kibondo kushughulikia tatizo hilo mara moja ili wananchi waweze kupata huduma bora ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wagonjwa wanaofika kutibiwa  MWISHO

No comments:

Post a Comment