Pages

Monday, November 19, 2012

Raia wa Nairobi Kenya aachiliwa huru katika mahakama ya wilaya ya kibondo baada ya ushahidi wa keshi yake kutojitosheleza



KIBONDO
Mtu mmoja mwenyeji wa wilaya ya Msoma mkoani Mara aliyedhaniwa kuwa ni raia wa Kenya ameachiliwa huru na mahakama ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma baada ya ushahidi kuwa ni raia wa Kenya kutojitosheleza

Mbele ya hakimu wa wilaya bw Erick Marley mwendesha mashitaka wa uhamiaji bw Njunwa Mlaki amemtaja mtu huyo kuwa ni bw Otieno Matara mwenye umri wa miaka 17

Bw Mlaki amesema kuwa bw Matara alikamatwa mjini kibondo Juni 26 mwaka huu majira ya saa nane na nusu mchana ambapo alitoa maelezo kwa afisa uhamiaji bw Rogatho Bartholomew kuwa yeye ni raia wa Tanzania

Aidha bw Mlaki amesema kuwa bw Matara alikuwa amefunguliwa mashitaka  ambapo kosa la kwanza lilikuwa ni kupotosha majukumu ya afisa uhamiaji kwa kutoa habari za uongo na kosa la pili lilikuwa ni kuishi nchini kinyume cha sheria

Baada ya ushahidi kuwa bw Matara ni raia wa Kenya kutojitosheleza hakimu wa wilaya ya kibondo bw Erick Marley amemuachilia huru mtuhumiwa huyo leo November 19, 2012   MWISHO 

No comments:

Post a Comment