MKAZI mmoja wa kijiji cha Kazilamihunda wilaya ya Kakonko mkoa wa kigoma amepigwa lisasi na kufariki dunia wengine saba kukimbilioa kusiko julikana baada ya kukutwa wanaiba Mabati katika kikosi 824 cha jeshi la kujenga Taifa Kanembwa
Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu akiwa na wenzake 8 walikutwa juu la paa la jengo moja huku wakibomoa mabati ndani ya kikosi hicho kwa kuezua mabati.ambapo wanajeshi walio kuwa dolia waliwabaini na kupiga Risasi ndipo ilimpata mmoja wao na wengine kukimbilia kusiko julikana.
Tukio hilo limetukia November 19 mwaka huu majira ya saa 6:00 usiku katika Kikosi cha 824 KJ,Kanembwa ambapo marehemu ametambuliwa kwa majina kuwa ni Mohozya Joakimu mwenye umri wa Miaka 25 mkazi wa Kijiji cha Kaziramihuda katika Wilaya mpya ya Kakonko.
Aidha kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma Bw. Freiser Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha tabia za uharibifu wa mali.za umma
Hata hivyo Kabla ya JKT kuingia na kuanza kufanya shughuli zake eneo hilo , mwanzoni lilikukuwa likitumiwa kama kambi ya kuhifadhi wakimbizi wa Burundi waliokimbia vita nchini mwao 1994.
Hali hiyo uwafanya wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka eneo hilo udhani kuwa bado kuna vitu ambavyo wanaweza kupata. Mwisho
No comments:
Post a Comment