Kijana aliyeng’atwa sehemu kubwa ya uso mwishoni mwa mwezi Novemba amepata upofu wa macho yote mawili pamoja na kwamba madonda makubwa yaliyoko usoni mwake yanaendelea kupona siku hadi siku
Mganga wa wodi ya wagonjwa majeruhi Dr. Victor Nzaro akiongea na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya kijana Susuruka aliyelazwa hospitalini hapo amesema kuwa majeraha yameanza kupona na anauwezo wa kutoka nje
Aidha Dr. Nzaro amesema kuwa suala la kupelekwa nje ya nchi kijana huyo kwa ajili ya matibabu zaidi litatolewa maamuzi na uongozi wa wilaya na kwamba macho ya kijana huyo tayari yamepofuka pamoja na kwamba vidonda vikubwa vilivyopo usoni mwa kijana huyo vinaendelea kupona siku hadi siku
Kwa upande wake bw Paul Kanani baba mzazi wa Iman Paul ambaye amemuuguza kijana huyo amesema kuwa ameanza kula chakula ambacho ni laini na hali ya yake kwa ujumla inaendelea vizuri ukilinganisha na siku za nyuma
MWISH O
No comments:
Post a Comment