Viongozi na wajumbe wa Halmashauri ya kijiji cha kibondo
mjini wametoa taarifa ya kujiuzuru nafasi yao kwa mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya kibondo ifikapo septemba 28 mwaka huu ikiwa halmashauri hiyo haitatafuta
ufumbuzi wa migogoro iliyopo kati ya kijiji hicho na halmashauri
Mwenyekiti wa kijiji cha kibondo mjini bw Robert Ntendeli
ameiambia KIBONDO MOTO kuwa uamuzi huo ulitolewa na wajumbe wa kikao kilichoketi agost 30 , 2013 na
kuthibitishwa na wajumbe 19 septemba 2 mwaka huu huku wajumbe watano wakiwa
ndio pekee hawakusaini barua hiyo
Bw Ntendeli amesema kuwa wajumbe wa halmashauri ya kijiji
cha kibondo mjini wamefikia hatua ya kutaka kujiuzuru kwa sababu zipatazo sita ambapo
sababu hizo ni pamoja na juhudi za halmashauri ya kijiji kupendekeza na
kufuatilia utayari wa mamlaka ya mkurugenzi kufanya marekebisho stahiki ili
kuwezesha halmashauri ya kijiji kutimiza wajibu wake wa kuchochea maendeleo ya
kijiji hazikupewa umuhimu stahiki na hivyo kuikatisha tamaa
Usajili wa kijiji cha kibondo mjini haukuzingatia matakwa
muhimu ya kisheria katika fungu la 22 la sheria namba 7 ya mwaka 1982 la uwepo
wa ardhi yenye mipaka inayojulikana na jitihada za kuanzisha mamlaka ya mji
mdogo kwa misingi ya mafungu ya 27 na 28 ya sheria ambalo ndilo lilikuwa
suruhisho
Sababu nyingine ni mji wa kibondo haukustahili kuwa na
halmashauri ya kijiji kinyume na sheria baada ya kutokuwa na ardhi yake na
kulazimika kutawaliwa kwa sheria za ardhi mbili tofauti namba 4 na 5 za mwaka
1999 hali ambayo kiutendaji inatatanisha
Bw ntendeli amesema kuwa sababu nyingine ya kutaka kujiuzuru
ni kuwa halmashauri ya kijiji imeshindwa kuendelea na utendaji wa kuingiliana
na ofisi ya mkurugenzi ikiwa ni pamoja na ugawaji wa ardhi , uuzwaji wa majengo
na utekelezaji hafifu wa miradi inayofanywa kwa masirahi binafsi katika eneo la
mji bila kushirikishwa
Halmashauri ya kijiji pia inahofia kuwajibishwa na mkutano
mkuu wa kijiji kwa misingi ya sheria katika vifungu vya 142 na 143 vya sheria
kwa kutotimiza wajibu wao huku wakizuwiya uwezekano wa kuendelea kwa kijiji kwa
kuhofia kuwaudhi viongozi wanaokinzana nao
Sababu ya mwisho ni kwamba halmashauri ya kijiji imekubali
kushindwa katika mvutano wa kimasirahi kati yake na uongozi wa kata na wilaya
baada ya kulidhika kwamba hakuna nia thabiti ya kuiwezesha kujiendesha baada ya
kunyimwa fursa kama zinazotolewa kwa vijiji vingine
Bw ntendeli amesema kuwa ikiwa sababu hizo zilizotajwa hazitakuwa zimepatiwa
ufumbuzi utakaokuwa umeulidhisha mkutano huo kabla ya septemba 28 mwaka huu halmashauri ya kijiji
cha kibondo mjini itatoa taarifa lasmi ya kujiuzuru nafasi yake kwa mkutano
mkuu wa kijiiji hicho
Blog yako ya nguvu KIBONDO MOTO bado inafanya juhudi za
kumtafuta mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kibondo bw Leopord
Chundu Ulaya ili kuzungumzia mwafaka wa mgogoro huo kati ya serikali ya kijiji na
halmashauri ya wilaya.
No comments:
Post a Comment