Pages

Wednesday, October 17, 2012

anusulika kufa baad ya kukatwa mapanga na watu wasiofahamika



Mkazi mmoja  Wilayani  Kibondo Mkoani Kigoma amenusulika kuuawa baada ya kukatwa katwa na mapanga kisha kutelekezwa katika poli lililoko nje kidogo ya mjij wa kibondo

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Wilayani kibondo zimemtaja aliyejeruhiwa kuwa ni Andason  Ruta ambaye ni mfanya biashara mkazi wa kibondo mjini na kwamba Tukio hilo limetokea jumatatu October 15 majira ya saaa mbili usiku wa kuamkia jumanne katika  kijijij cha nabuhima nje kidogo ya mji wa kibondo

Akiongea na radio kwizera akiwa katika hospitali ya wilaya ya kibondo bw Underson Ruda amesema kuwa akiwa nyumbani kwake alipigiwa simu na watu asiowafahamu  kwamba wanataka kufanya nae biashara ya mashine ya kusaga ndipo walipomchukua mpaka katika poli lilopo nje kidogo ya mji wa kibondo kwa ajili ya kumfanyia unyama huo

Taarifa zinasema kuwa  hakuna mtu yoyote anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo  kutokana na majeruhi huyo kusema kuwa hakuweza kumfahamu mtu yeyote wala gari lililotumika katika tukio hilo 

Aidha jeshi la polisi limemtilia mashaka bw Anderson kwa kuwa ni vigumu kupigiwa simu na mtu usiyemfahamu kasha ukaenda bila kuhoji aliyekuita ni nani na anataka nini
aidha jeshi hilo limesema kuwa huenda mtu huyo alikuwa anapanga njama na watu hao ndipo wakashindwa kuelewena kabla ya kutokea kwa tukio hilo 

Kaimu mganga mkuu wilayani kibondo bw Thomas Bahufasha amesema kuwa bw Anderson alikatwa na kitu chenye ncha kali katika maeneo ya kichwani begani pamoja na kwenye paja na kwamba mgonjwa huyo anaendelea vizuri na matibabu hospitalini hapo   MWISHO

No comments:

Post a Comment