Mkazi wa kata ya mabamba wilayani kibondo mkoani kigoma
ameokota siraha aina ya SMG alipokuwa akilima shambani kwake ikiwa na lisasi 26
pamoja na magazine moja kisha kuisalimisha serikali ya kijiji
Siraha hiyo imeokotwa na mkazi wa kitongoji cha Kijangala
kijiji cha Mkalazi kata ya Mabamba bw Moshi Razalo mwenye umri wa miaka 24
jumanne hii ya Novemba 19 ambapo siraha hiyo ilikuwa imefungwa kwenye suruali
ya kijeshi kisha kuchimbiwa ardhini
‘’Nilikuwa nalima shambani kwangu sasa nikasikia kama jembe
linakwama kwenye kitu kigumu nilipofukua ndio nikaona suruali ya kijeshi
kuangalia nikakuta kuna siraha pamoja na lisasi zipatazo 26 basi ikabidi
nivisalimishe serikali ya kijiji alisema bw Moshi Razalo
Aidha Bw Razalo amesewataka raia wema kusalimisha siraha
ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mara tu waonapo ama
kuhisia mtu yeyote mwenye kumliki siraha kinyume cha sheria ili kuimarisha
usalama wa raia na mali zake kwa maendeleo ya jamii
Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto pamoja na mkuu
wa jeshi la polisi bw Marko Joshua walipigiwa simu mara baada ya siraha hiyo
kusalimishwa kwa serikali ya kijiji kisha kuchukua uamuzi wa kuifuata siraha
hiyo na kuihifadhi kituo cha polisi
kibondo
‘’ ilibidi nimpigie simu mkuu wa jeshi la polisi wilayani
hapa kisha tukaenda eneo la tukio tukamkuta kijana aliyeokoto bunduki hiyo
akaeleza jinsi ilivyokuwa kwa kweli anaonekana ni mzalendo na mimi nitampa
motisha ya shilingi elfu 50 ili iwe fundisho kwa wengine unajua SMG ni siraha
ya kivita kabisa kwa hiyo kama mtu mwingine angeenda kuitumia tofauti kabisa
alisema bw Mwamoto
BW razalo amepatiwa motisha ya shilingi elfu hamsini baada
ya kuokota siraha hiyo na kuisalimisha ikiwa ni motisha kwake na kwa watu
wengine watakaoona au kutoa taarifa za watu wanaomiliki siraha kinyume cha
sheria ENDS
No comments:
Post a Comment