Pages

Wednesday, November 6, 2013

MUNGU MKUBWA susuruka bado anaishi !!!!!!!!!!!!!!



KIBONDO

Matumaini ya kuweza kutembea tena  Mkazi wa wilaya ya kakonko aliyelazwa katika hospitali ya wilaya ya kibondo kwa zaidi ya miaka sita baada ya kuvunjika uti wa mgongo  na baadae kuhamishiwa katika hospitali ya Bugando iliyoko jijini Mwanza yamefifia na badala yake juhudi  zinaendelea kufanywa na madaktari ili angalau aweze kukaa

Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto ambaye ndiye aliyefanikisha mpango wa bw Razalo Paulo pamoja na susuruka kupewa rufaa ya kwenda kutibiwa ameiambia radio kwizera kuwa bw razalo hataweza kupona uti wa mgongo baada ya kuchelewa sana kupewa rufaa ya kwenda kutibiwa hospitali kubwa  

Aidha bw Mwamoto amesema kuwa bw Razalo amepewa rufaa nyingine kutoka bugando  jijini mwanza kwenda KCMC iliyoko mkoani Kilimanjaro  na kwamba kijana susuruka aliyeng’atwa sehemu kubwa ya uso wake yeye amepewa rufaa yak wenda muhimbili jijini dar es salaamu ambako anaendelea na matibabu ya kawaida kabla ya kusafirishwa kwenda nje kwa matibabu zaidi

Bw mwamoto amesema kuwa mpango wa kufungua account benk kwa ajili ya kuwachangia wagonjwa hao ulishindikana na yeyote ambaye angependa kuwachangia ili waweze kupata matumizi madogo madogo wanaweza kufika ofisi ya mkuu wa wilaya kibondo au kwenda hospitali ya wilaya na kuonana na mganga mkuu

Akiongea na radio kwizera kwa njia ya simu bw Razalo Paulo amewaomba wananchi  kuendelea kumchangia pesa za matumizi madogo madogo kupitia namba yake ya simu 0764008846 na kwamba hali yake pamoja na kwamba hajawahi kukaa tangu mwaka 2006 alipopata ajali  inaendelea vizuri

Kijana susuruka yeye alingatwa sehemu kubwa ya uso wake na mwajili wake aitwaye imani Paulo  ambaye mpaka hivi sasa anatumikia kifungo katika gereza la wilaya ya kibondo na razalo Paulo alianguka na kuvunjika uti wa mgongo tangu mwaka 2006 hali iliyopelekea alazwe katika hospitali ya wilaya ya kibondo kwa zaidi ya miaka 6 akiwa hana uwezo wa kusimama wala kukaa mpaka hivi sasa

No comments:

Post a Comment