Diwani wa kata ya kumsenga wilayani kibondo mkoani kigoma bw
Saimon Kanguye ametoa wito kwa wazazi kutambua faida ya elimu ikiwa ni pamoja
na kujenga utamaduni wa kuwahimiza
watoto wao kwenda shule kwa kuwa elimu ndio mkombozi wa masikini
Bw Kanguye ametoa wito huo katika mkutano wa hadhara
aliouitisha katika kijiji cha Kibuye kata ya Kumsenga baada ya zahanati ya
kijiji hicho kuwa na upungufu wa watumishi huku shule ya msingi ya kijiji hicho
ikiwa haijawahi kuwa na mwalimu mzawa
Bw Kanguye amesema kuwa kwa hivi sasa vijana wengi
wamejiingiza katika swala zima la matumizi ya madawa ya kulevya hali
inayosababisha kupoteza ndoto na malengo ya baadae hivyo wazazi wanapaswa kuwa
makini ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha watoto wao juu ya athali za matumizi ya
madawa ya kulevya
No comments:
Post a Comment