Mbunge wa jimbo la muhambwe bw Felix Mkosamali amezuia
wananchi kujiandikisha kwa ajiri ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika kituo
cha sekondari murungu kijiji cha Kumuhasha akishinikiza halimashauri kuruhusu
wananchi wa kijiji cha Nduta kambini kuruhusiwa kujiandikisha katika kituo
hicho baada ya kutokuwa na kituo cha kujiandikisha kijijini kwao
Bw Mkosamali ametoa agizo hilo akiwa katika kituo hicho mapema hii leo
novemba 24 , ambapo alikuta karani mwandikishaji akikataa kuwaandika wananchi
ambao ni wakazi wa kijiji cha nduta kambini kwa madai kuwa ni maagizo aliyopewa
na afisa mtendaji wa kijiji hicho
Aidha bw Mkosamali amesema kuwa wananchi wa kijiji cha Nduta
kambini kama walivyo wananchi wengine wanahaki
ya msingi kikatiba ya kuchagulia na kuchagua kiongozi wanayemtaka na kwamba
hizo ni hujuma za chama cha mapinduzi wakitaka wananchi wa kijiji hicho
wasipate fursa ya kuchagua na kuchaguliwa
Baadhi ya wananchi waliokumbwa na mkasa huo wamesema kuwa
wameshindwa kujiandikisha baada ya kukataliwa kwa madai kuwa wao hawapaswi
kujiandikisha katika eneo hilo
kwa kuwa sio kijiji chao
Kwa upande wake karani mwandikishaji wa kituo hicho bw Kadiri
Hamidu amesema kuwa yeye anafuata maelekezo aliyopewa na afisa mtendaji wa
kijiji hicho kwamba hapaswi kuwaandika wananchi wanaokaa nduta kambini
Nae afisa mtendaji wa kijiji cha kumuhasha bw meshaki
mavukilo alipoulizwa swala hilo
amesema kuwa maelekezo aliyopewa ni kuwa kila mwana kijiji anapaswa
kujiandikisha katika kijiji anachokaa kwa maana hiyo wakazi wa nduta hawapaswi
kujiandikisha katika kijiji hicho
msimamizi wa uchaguzi
bw Fedi Eliasafi amesema kuwa wananchi wa kijiji cha Nduta kambini wanapaswa
kujiandikisha katika vijiji walivyotokea kwa kuwa hakuna kijiji cha Nduta
kambini na kwamba hakuna kituo cha kuandikisha wananchi katika kijiji hicho
ENDS
No comments:
Post a Comment